IQNA

Mawahhabi wapinga mapatano ya nyuklia ya Iran

17:22 - January 18, 2016
Habari ID: 3470059
Wanazuoni 140 wa pote la Uwahhabi wametoa taarifa ya kupinga mapatano ya nyuklia ya Iran ambayo yalianza kutekelezwa Jumamosi.

Katika taarifa, Mawahhabi hao wameonya kuhusu kile walichodai kuwa eti ni ‘tishio la Iran’ na kudai kuwa ni jukumu la Waislamu kukabiliana na tishio hilo.

Pote la Uwahhabi linafuata misimamo ya kufurutu ada na wafuasi wa pote hilo ndio wanaotawala Saudi Arabia. Itikadi ya Uwahhabi inafuatwa pia na makundi mengi ya kigaidi duniani kama vile Daesh au ISIS, Boko Haram la al Shabab.

Ikumbukwe kuwa hatimaye mapatano ya nyuklia ya Iran yajulikanayo kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA) umeanza kutekelezwa. Kwa mujibu wa ripoti ya pamoja iliyotolewa jana na Mohammad Javad Zarif, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran na Federica Mogherini, Mkuu wa Sera za Nje wa Umoja wa Ulaya huko mjini Vienna, Austria, vikwazo vyote vya kifedha, uchumi na vinginevyo vinavyohusiana na mpango wa nyuklia wa Iran vimeondolewa rasmi kuanzia tarehe 16, Januari mwaka huu, kwa mujibu wa makubaliano hayo ya nyuklia. Mapatano hayo ni baina ya Iran na madola sita makubwa duniani katika kundi la 5+1 ambalo linajumuisha Russia, China, Uingereza, Ufaransa, Marekani na Ujerumani.

Katika hali ambayo aghalabu ya wapenda amani duniani hasa mataifa ya Waislamu wamekaribisha mapatano hayo ya nyuklia, lakini baadhi ya tawala na vibaraka wao hasa Mawahhabi wamepinga mapatano hayo. Wapinzani wakubwa wa mapatano hayo katika eneo ni utawala wa Kizayuni wa Israel na utawala wa kifalme Saudia. Tawala hizo mbili ni maarufu kama waungaji mkono wa makundi ya kigaidi kote duniani.

3468260

captcha