IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Kuna ulazima kuwa macho kuhusu hadaa za Marekani

18:56 - January 21, 2016
Habari ID: 3470074
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema kuwa mahudhurio makubwa ya wananchi wa Iran katika uchaguzi wa tarehe 26 Februari hapa nchini yatadumisha amani na heshima ya taifa la Iran na kudhamini ustawi na maendeleo ya Jamhuri ya Kiislamu.

Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo Jumatano mjini katika hadhara ya maafisa wanaosimamia zoezi la uchaguzi wa awamu ya 10 ya Bunge la Iran na awamu ya tano ya Baraza la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi Muadhamu. Ameeleza sababu zinazodhamini ushindani sahihi katika uchaguzi na kusema kuwa, taifa na Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ndiye mshindi mwenye fahari kubwa wa ushindani wa kitaifa na mkubwa katika medani ya uchaguzi.

Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amezitaja chaguzi mbili zijazo hapa nchini kuwa zina umuhimu mkubwa na kuongeza kuwa: Sharti muhimu zaidi la uchaguzi salama ni kushiriki watu wote waliokamilisha masharti ya kupiga kura hata wake wenye hitilafu na mfumo unaotawala hapa nchini.

Ayatullah Khamenei ameashiria njama zinazofanywa na baadhi za kutaka kuwazuia watu kushiriki katika uchaguzi, kususia zoezi hilo au kudhoofisha uchaguzi huo na kusema: Taifa la Iran limeonesha msimamo wake mbele ya watu wa namna hii.

Amesisitiza udharura wa vyombo na maafisa wote kuheshimu sheria, kutotia tashwishi katika fikra za wananchi, wagombea kutovunjiana heshima, kujiepusha na kusengenya, kutotoa ahadi zisizotekelezeka na kuamiliana na wananchi kwa ikhlasi na ukweli kuwa ni miongoni mwa masharti ya uchaguzi sahihi na salama.

Ayatullah Khamenei pia amemshukuru Rais wa Jamhuri, Waziri wa Mambo ya Nje na wananchama wote wa timu ya Iran katika mazungumzo ya nyuklia kuhusu suala la kutatuliwa faili la nyuklia la Iran na kusema: Hata hivyo matakwa yote ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hayakutimizwa, lakini maafisa husika wamefanya jitihada kubwa katika uwanja huo.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza masuala muhimu yanayohusiana na utekelezaji wa makubaliano ya nyuklia kati ya Iran na kundi la 5+1 na kuwaambia maafisa wa serikali kwamba: Marekani ndiyo ile ile Marekani ya zamani, kwa msingi huo kuna ulazima wa kuwa macho mbele ya hadaa zake katika utekelezaji wa makubaliano hayo.

Ayatullah Khamenei amesema matunda ya nyuklia ni matokeo ya juhudi na umahiri wa wasomi wa Iran na uungaji mkono wa taifa; hivyo si insafu kwa baadhi ya watu kueneza propaganda kuwa matunda haya ni matokeo ya fadhila za Marekani!

Akiashiria sifa nyingine ya Marekani, Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu amesema: Matukio ya sasa katika eneo la Mashariki ya Kati yameweka wazi malengo na makusudi ya miaka kadhaa iliyopita ya Wamarekani ya udharura wa kuanzishwa Mashariki ya Kati mpya; kwani Mashariki ya Kati mpya ya Wamarekani ni Mashariki ya Kati yenye vita, ugaidi, chuki na taasubi na iliyojaa mapigano ya kimadhehebu na ya ndani.

3468942

captcha