IQNA

Al Azhar Kuanzisha Televisheni ya Kiingereza na Kifaransa

16:46 - May 29, 2016
Habari ID: 3470343
Sheikh Ahmad Tayyib, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Al Azhar cha Misri amesema chuo hicho kitaanzisha televisheni ya satalaiti itakayorusha matangazo kwa lugha za Kiingereza na Kifaransa ili kuwasilisha taswira sahihi ya Uislamu katika nchi za Magharibi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikhe Mkuu wa Al Azhar Ahmad Tayyib katika kikao baina yake na Mkuu wa Baraza la Waislamu Ufaransa Jumapili katika Ubalozi wa Misri mjini Paris, amesema: "Katika fremu ya jitihada za Al Azhar za kupambana na misimamo mikali na kuwasilisha taswira sahihi ya Uislamu hasa katika jamii za Magharibi, Al Azhar itaanza kanali ya televisheni ya satalaiti kwa lugha za Kiingereza na Ufaransa katika kipindi cha mwaka moja ujao."

Aidha kiongozi huyo wa Al Azhar ametahadahrisha kuhusu baadhi ya wahubiri bandia ambao wanachafua sura ya Uislamu kwa tabia zao. Amesema Waislamu waliowacahche katika nchi za Ulaya wanaweza kuwa na mchango mkubwa katika kuarifisha Uislamu asili na halisi.

Aidha ametoa wito kwa Waislamu Ulaya kuweka kando hitilafu zao kwani iwapo watalumbana basi hawawezi kutarajia wengine wawe na mtazamo mzuri kuhusu Uislamu.

Sheikhe Mkuu wa Al Azhar katika safari yake ya kwanza rasmi nchini Ufaransa amekutana na Rais Francois Hollande wan chi hiyo pamoja na spika wa bunge la nchi hiyo.

Wiki iliyopita Sheikh Tayyib alikutana na Papa Francis, Kiongozi wa Kanisa Katolki Duniani huko Vatican ambapo walikubaliana kuandaa kongamano la kimataifa la Amani.

3501945
captcha