IQNA

Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran

Waislamu wawe na umoja kupambana na ugaidi, misimamo mikali

11:03 - June 22, 2016
Habari ID: 3470408
Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran Muhammad Javad Zarif amesema Waislamu wanapaswa kuungana ili kuonyesha nchi za Magharibi kuwa wanaweza kupambana na ugaidi na misimamo mikali ya kidini.
Zarif ameyasema hayo Jumanne usiku mjini Paris Ufaransa na kuongeza kuwa, ugaidi umeathiri vibaya Waislamu na nchi za Kiislamu duniani. Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran amebaini kuwa, badala ya Waislamu kuchochea tafauti baina yao, wanapaswa kuoneysha namna ya kukabiliana na changamoto zinazoukumba Uislamu na pia washirikiane katika kustawisha mataifa ya Kiislamu na jamii za Waislamu kote duniani.

Zarif ameyasema hayo katika dhifa ya futari iliyowaleta pamoja wanadiplomasia wa nchi za Kiislamu na wawakilishi wa jumuiya za Kiislaamu barani Ulaya katika makao ya balozi wa Iran mjini Paris.

Waziri wa Mambo ya Nje ya Iran amesema kwa mujibu wa mafundisho ya Kiislamu, anayeua mtu asiye na hatia ni kama ameua wanadamu wote na kwa msingi huo Waislamu wanapaswa kuuarifisha Uislamu kama dini ya wanadamu wote.

Aidha ameashiria kudhulumiwa Waislamu huko Palestina na kusema Waislamu wanapaswa kuungana kuwatetea Wapalestina.
/3460171
captcha