IQNA

Mwanamke Mwislamu alazimishwa kuvua Hijabu akitafuta kazi New Zealand

9:36 - July 26, 2016
Habari ID: 3470475
Mwanamke Mwislamu mwenye umri wa miaka 25 amedhalilishwa baada ya kunyimwa kazi kutokana na vazi lake la Hijabu.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mona Alfadli, aliomba kazi kama muuzaji bidhaa katika duka la dhahabu  la Steward Dawsons huko Auckland, New Zealand na kufahamishwa na mkurugenzi wa duka hilo kuwa asijitaabishe kuomba kazi kwa sababu amefaa Hijabu. Mona amesema amedhalilishwa na kitendo hicho na kwamba tokea awali alihisi kuwa atanyimwa kazi hiyo.

Alfadli, ambaye anaishi Avondale, amekuwa akitafuta kazi baada ya kupata cheti cha diploma katika uhandisi wa kompyuta. Anaongeza kuwa, amekuwa na ndoto ya kuboresha maisha yake na familia yake nchini New Zealand baada ya kupewa hifadhi nchini humo mwaka 2008 akitokea Kuwait.

"Ninaweza kufanya kila aina ya kazi, lakini lazima nivae vazi la Hijabu. Nitalinda utambulisho wangu, nitaheshimu utamaduni na dini yangu,” amesema Alfadli alipohojiwa na gazeti la The New Zealand Herald.

Hii ni mara ya pili kwa mwanamke Mwislamu kazi kutokana na vazi la Hijabu Australia. Oktoba mwaka jana, naibu mkuu wa zamani Chuo cha Wasichana cha Kelston Fatima Mohammadi alinyimwa kazi katika duka la dhahabu la Henderson kwa sababu ya vazi lake la Hijabu.

Mwaka 2015, mwanamke Mwislamu Mmarekani Samantha Elau alishtaki na kufanikiwa katika kesi dhidi ya Shirika la Abercombie & Fitch ambalo lilimnyima kazi kutokana na vazi lake la Hijabu.

Kumekuwepo na kesi nyingi za wanawake Waislamu kudhalilisha, kunyimwa kazi na hata haki ya elimu katika nchi za Magharibi kutokana na vazi la Hijabu. Hatua hizo ni katika wimbi la chuki dhidi ya Uislamu katika nchi za magharibi.

3460497

captcha