IQNA

Zakir Naik, mhubiri wa Kiwahhabi kupigwa marufuku India

21:33 - October 28, 2016
Habari ID: 3470639
Serikali ya India inapanga kupiga marufuku Taasisi ya Utafiti wa Kiislamu (IRF) inayosimamiwa na mhubiri mwenye utata wa pote la Kiwahhabi, Zakir Naik.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, gazeti la Hindustan Times limeandika kuwa Zakir Naik ambaye ana misimamo mikali na anayetambuliwa kuwa kiongozi wa Mawahhabi nchini India anamiliki pia televisheni iitwayo 'Peace TV' ambayo inahusika na uenezaji fikra za Uwahhabi. Afisa mwandamizi wa Wizara ya Mambo ya Ndani India ambaye hakutaja jina lake litajwe amesema, "Tunatayarisha taarifa ya kupiga marufuku IRF kwa mujibu wa Kipengee cha 3 cha Harakati Zilizo Kinyume cha Sheria. Uchunguzi wa mwisho unafanyika kabla ya kupata idhini ya baraza la mawaziri."

Iwapo uamuzi huo utapitishwa, itamaanisha kuwa hakuna mtu anayeweza kuwa mwanachama wa IRF au kufadhili taasisi hiyo. Aidha mali zote za taasisi hiyo ya Kiwahhabi zitatangazwa kuwa haramu na kudhibitiwa na serikali.

Mwezi Julai serikali ya nchi za Kiislamu ya Bangladesh iliipiga marufuku televisheni ya satalaiti ya 'Peace TV' inayofungamana na mhubiri wa Kiwahhabi Zakir Naik kwa tuhuma za kuunga mkono misimamo mikali na ugaidi. Julai 10 serikali ya Bangladesh ilitoa amri ya kusitishwa matangazo ya televisheni ya satalaiti ya Peace TV yenye makao yake Dubai. Serikali ya Bangladesh imesema televisheni za nchini humo hazina idhini tena ya kurusha matangazo ya Peace TV kutokana na kuwa televisheni hiyo inaeneze misimamo mikali ya kigini na kuhumiza harakati za kigaidi kupitia mawaidha na hotuba ambazo hutolewa na Zakir Naik, kiongozi wa Mawahhabi nchini India.

Tayari Zakir Naik ameshapigwa marufuku kuingia Uingereza na Canada na Peace TV imepiga marufuku katika nchi ya Kiislamu ya Malaysia.

Kati ya washambuliaji wawili ambao waliua watu 20 Julai 1 mjini Dhaka, Bangladesh wanasemekana kuwa wafuasi wa Zakir Naik katika mitandao ya kijamii.

Aidha kuna taarifa kuwa, vijana kadhaa wa India walichochewa na hotuba za Zakir Naik na kuelekea Syria kujiunga na kundi la kigaidi la ISIS. Peace TV ilianzishwa mwaka 2006 na inarusha matangazo yake katika nchi za Asia, Ulaya, Afrika, Australia na Amerika ya Kaskazini. Ina matangazo kwa lugha za Kiurdi, Banglad, Telugu na Malayalam. Peace TV imekuwa ikieneza chuki na itikadi za kuwakufurisha Waislamu wa madhehebu zigine wasiofuata pote la Uwahhabi.

3541348

captcha