IQNA

Japan yatenga vyumba vingi vya Waislamu kuswali

0:12 - November 07, 2016
1
Habari ID: 3470661
IQNA-Nchini Japan kumeshuhudiwa ongezeko la vyumba maalumu kwa ajili ya Waislamu kusimamisha sala katika maeneo ya umma.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Japan imechukua hatua za kuwavutia Waislamu wanaoishi au kuitembelea nchi hiyo kwa kuhakikisha wanapata maeneo ya kuswali na pia chakula halali.

Hatua hiyo imekuja kufuatia ongezeko kubwa la watalii, wafanyabiashara na wanafunzi kutoka nchi za Kiislamu wanaotembelea Japan.

"Wanafunzi wengi Waislamu wana hamu ya kusoma Japan,” amesema afisa wa chuo kikuu kimoja ambaye hakutaka jina lake litajwe. "Kuna mashindano miongoni mwa vyuo vikuu kuhusu njia za kuandaa mazingira ya kuwavutia wanafunzi Waislamu.”

Chuo Kikuu cha Rikkyo cha eneo la Toshima mjini Tokyo, kimetangaza mpango wa kuongeza idadi ya wanafunzi wasio kuwa Wajapani kufika 2,000 ifikapo mwaka 2024. Katika mojawapo ya hatua zilizochukuliwa chuoni hapo kuwavutia wanafunzi Waislamu ni kufunguliwa chumba maalumu cha kuswali mwezi Aprili mwaka huu. Chumba hicho kina nembo inayoonyesha qibla na pia eneo maalumu la kutawadha.

Mkuu wa Chuo Kikuu cha Rikkyo Tomoya Yoshioka anasema kufunguliwa chumba hicho pia kutakuwa ni fursa kwa wanafunzi wa Kijapani kujifunza kuhusu utamaduni wa Kiislamu.

Wakati huo huo Shirika la Utalii Japan linasema kumeshuhudiwa ongezeko la watalii kutoka nchi za Kiislamu za Malaysia na Indonesoa. Kuna watalii karibu nusu milioni wa nchi hizo mbili waliotembelea Japan mwaka 2014 na idadi hiyo inatazamiwa kuongezeka mara nne katika muongo ujao. Kwa msingi huo hoteli nyingi nchini Japan zimeanza kutoa huduma halali ambazo zinajumuisha chakula halali, chumba maalumu cha sala na vyumba vyenye ishara ya qibla.Japan yatenga vyumba vingi vya Waislamu kuswali

Aidha huku Japan ikijitayarisha kuandaa mashindano ya Olimpiki mwaka 2020, nchi hiyo imeanzisha mkakati wa kuimarisha maeneo yenye vyakula na huduma halali hasa mji mkuu Tokyo ambao utakuwa mwenyeji wa michezo hiyo.

Halikadhalika viwanja kadhaa vya kimataifa vya ndege nchini Japan vimetenga vyumba maalumu vya Waislamu kutumia wakati wa sala.

3461320

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
ussi
0
0
ni safi sana,nuru ya Allah na mafunzo ya mtume MUHAMMAD YATAENEYA KATIKA ULIMWENGU HUU,JAPO WASHIRIKINA WANACHUKIYA.
captcha