IQNA

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu

Magaidi wa Kitakfiri kwa mara nyingine wameonyesha uso wao khabithi na wa kishetani

18:48 - November 26, 2016
Habari ID: 3470700
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisistiza kuwa makundi yatendayo jinai ya kitakfiri, kwa mara nyingine yametekeleza hujuma kwa woga na kwa njia ya kuogofya na hivyo kuonyesha uso wao khabithi na wa kishetani kwa wote

Ayatullah Ali Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameyasema hayo katika ujumbe wake leo Jumamosi kufuatia tukio chungu na la kusikitisha ambapo makumi ya wafanyaziara waliuawa wakiwa katika safari ya ziara ya Bwana wa Mashahidi, Imam Hussein AS.

Katika ujumbe wake, Kiongozi Muadhamu ameongeza kuwa, matembezi adhimu ya Arubaini ya Imam Hussein AS na usalama wa kipekee katika matembezi hayo,ni mambo ambayo yameyapofusha makundi yatendayo jinai na uhalifu ya kitakfiri na kuvunja njama zao khabithi.

Siku ya Alkhamisi iliyopita, kufuatia hujuma ya trela la mafuta lililokuwa limesheheni bomu katika kituo cha petroli cha eneo la Al Shumali katika mji wa Hilla mkoani Babol kusini mwa Baghdad, Iraq, wafanya ziara zaidi ya 100 waliuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa. Idadi kubwa ya wafanyaziara waliouawa shahidi katika hujuma hiyo ambayo kundi la kigaidi la ISIS (Daesh) lilidai kuhusika nayo, walikuwa Wairani.

Ayatullah Khamenei amesema katika maeneo mengine ya dunia kama vile Nigeria, Pakistan na Afghanistan pia kuliripotiwa habari chungu na za kushtusha za jinai kama hiyo jambo ambalo linawatahadharisha Waislamu wote na wanaoumizwa na matukio kama hayo kuhusu hatari ya makundi ya kitakfiri na serikali zinazowapa himaya.

Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu halikadhalika amewaombea maghufira ya Mwenyezi Mungu na dua ya kupona haraka wasafiri na wafanyaziara wa Imam Ridha ASwaliopoteza maisha katika ajali ya treni hapa nchini. Katika ujumbe wake, Kiongozi Muadhamu amewataka maafisa husika ndani na nje ya nchi kutoacha matukio hayo mawili yapite bila kushughulikiwa na wajitahidi kuwatibu majeruhina kuwasafirisha waliopoteza maisha sambamba na kupunguza masaibu ya waliokumbwa na msiba.

Watu zaidiya 50walipoteza maisha na wengine 100 kujeruhiwa Ijumaa ya jana katika ajali ya treni mbili iliyotokea katika mkoa wa Semnan mashariki mwa Tehran.

3548948

captcha