IQNA

Magaidi wa ISIS (Daesh) wabomoa misikiti 104 Mosul, Iraq

11:17 - December 10, 2016
Habari ID: 3470730
IQNA: Magaidi wakufurishaji wa kundi la ISIS (Daesh) wamebomoa misikiti 104 katika mji wa Mosul nchini Iraq katika mapambano yanayoendelea sasa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Abubakr Kanaan mkurugenzi mkuu wa Waqfu wa Ahul Sunna katika mkoa wa Nineveh kaskazini mwa Iraq amesema tokea mwezi Juni mwaka 2014 wakati magaidi wa ISIS walipoukalia kwa mabavu mji wa Mosul hadi sasa, wembomoa misikiti 104. 

Ameongeza kuwa mioni mwa misikiti hiyo 37 imebomolewa na magaidi hao wa Kiwahhabi kutokana na kuwepo makaburi ndani yake. Halikadhalika afisa huyo wa Waqfu amesema misikiti mingine 67 imebaribiwa kwa mabomu na magaidi wa ISIS na aghalabu haiwezi tumika tena kutokana na uharibifu mkubwa na hivyo inapaswa kujengwa upya.

Kanaan amesema magaidi wa ISIS wameharibu maeneo mengi ya kihistoria na turathi muhimu za Kiislamu mjini Mosul, mji wenye historia ndefu.

Magaidi wa Kiwahabbi wa ISIS waliianzisha kampeni ya ukatili nchini Iraq mnamo Juni 2014 wakati walipouvamia na kuuteka mji wa Mosul. Magaidi hao wametekeleza jinai za kinyama dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni, Shia  na pia Wakristo katika maeneo waliyoyateka Iraq. Serikali ya Iraq inasema baadhi ya nchi jirani kuwa ndizo zinazounga mkono kundi la ISIS.
captcha