IQNA

Waislamu wawili wafukuzwa kutoka ndege ya Marekani kwa kuzungumza Kiarabu

11:33 - December 22, 2016
Habari ID: 3470753
IQNA-Waislamu wawili wametimuliwa kutoka ndege ya shirika moja la Marekani mjini London baada ya wasafiri kadhaa Waingiereza kulalamika kuwa walimsikia mmoja wao akizungumza kwa lugha ya Kiarabu kwa simu.

Adam Saleh ambaye na rafiki yake Salim Albaher walikuwa wakirejea mjini New York Jumatano wakati walipotakiwa na robani wa ndege ya Shirika la Delta kuondoka katika ndege hiyo hiyo iliyokuwa katika Uwanja wa Heathrow mjini London.

Saleh mwenye umri wa miaka 23 anasema baadhi ya wasafiri walifungamana naye na kupinga hatua ya rubani huku baadhi wakishangilia alipotimuliwa kutoka katika ndege hiyo.

Salehi, ambaye amesema alikuwa akizungumza na mama yake mzazi kwa lugha ya Kiarabu, ametuma taswira ya video kuhusu tukio hilo kupitia mtandao wake wa twitter. Idadi kubwa ya watu wamebainisha ghadhabu yao katika mitandoa ya kijamii kufuatia tukio hilo la kibaguzi.

Katika video hiyo, Saleh anasikika akisema: "Nyingi ni wabaguzi, siamini ninachokiona. Wazungu sita dhidi ya watu waweli wenye ndevu. Huu ni mwaka 2016, 2016. Tizama Shirika la Delta linatutumua kwa sababu tu tunazungumza lugha tafauti."

Baada ya kuchelewa kwa masaa kadhaa, Saleh anasema hatimaye walifanikiwa kupanda ndege ya kuelekea New York lakini kwa kufanyikwa uchunguzi mkali wa kiusalama.

Amesema atachukia hatua za kisheria dhidi ya Shirika la Delta.

Katika miezi ya hivi karibuni kumeripotiwa visa kadhaa vya Waisani na Waarabu katika nchi za Magharibi wametakiwa waondoke ndani ya ndege kwa sababu ya dini yao.

3555788

captcha