Ayatullah Khamenei, Kiongozi Muadhamu wa
Mapinduzi ya Kiislamu ameyasmea hayo leo Jumapili hapa mjini Tehran wakati
alipokutana na maelfu ya wakaazi wa Qum na kuongeza kuwa maadui asili wa kigeni
si nara bali ni ukweli wenye nyaraka na ushahidi. Ameongeza kuwa: "Waziri
wa Mambo ya Nje wa Marekani anayataja kuwa eti ni 'mwenye muamala mwema' katika
barua yake ya kuaga ameishauri serikali ijayo nchini humo, 'ichukue hatua
kali dhidi ya Iran na iendeleze vikwazo kwani kwa hatua hizo kali itaweza
kulegeza misimam ya Iran." Amesema huyu adui mwenye kutabasamu hana
tafauti hata kidogo na yule aliyeitaja Iran kuwa mhimili wa shari.
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu
ameashiria uadui wa 'Waingereza' na kusema: "Uingereza ni mkoloni mkongwe
aliyechakaa na sasa kwa mara nyingine amekuja katika Ghuba ya Uajemi kwa lengo
la kuzitumia nchi za eneo hili kwa maslahi yake na ni kwa sababu hii ndio maana
katika hali ambayo yeye ndiye tishio halisi anadai kuwa eti Iran ndiyo
tishio."
Kiongozi Muadhamu ameendelea kusema kuwa:
"Uingereza inapanga na kuchukua maamuzi kwa ajili ya nchi za eneo hili
ikiwemo Iran na moja ya malengo yake ni kuzigawa vipande vipande nchi za
Iraq, Syria, Yemen na Libya na ina nia hiyo hiyo kuhusu Iran lakini kwa kuhofia
fikra za umma, nchini Iran hailitaji lengo hilo wazi wazi."
Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya
Kiislamu amesema, Waingereza wanasema wanatekeleza mpango kwa ajili ya
vizingiti na vikwazo vya baada ya mapatano ya nyuklia ya Iran na pia wanatoa
mafunzo na kuwapa silaha wenyeji wa eneo hili wakiwemo walioko Iran ili
waweze kutoa pigo kwa mfumo wa Kiislamu na taifa.
Ayatullah Khamenei ameashiria mpango na
njama za majopo ya kifikra ya Marekani na Uingereza katika kukabiliana na
"dini ya kisiasa' huku wakiwa na mpango wa 'kutenganisha dini na
siasa na kusema: "Wanalenga kuhakikisha kuwa dini inabakia ndani ya
misikiti na ndani ya nyumba na kuifanya dini iwe jambo la mtu binafsi huku
wakipinga dini ambayo inaenda sambaba na hatua za kivitendo katika
massuala ya uchumi na siasa. Aidha wanataka dini ambayo inasalimu amri mbele ya
adui."
Kiongozi Muadhamu amesisitiza kuwa, adui
anaogopa dini ambayo ina uwezo wa kusimamia masuala ya serikali, uchumi, siasa,
nguvu, jeshi na mfumo wa kifedha na kiidara. Kwa msingi huo amesema maarifa
sahihi ya dini ni yale ambayo hayatenganishi dini, maisha na siasa.
Kiongozi Muadhamu ameashiria namna adui
hakulifahamu vizuri taifa la Iran katika fitina za mwaka 2009 na kusema fitina
hizo ni mfano wa wazi wa makosa katika mahesabu ya adui. Ameongeza kuwa katika
mwaka huo kwa kuzusha fitna mwaka huo, adui alidhani anaelekea kupata mafanikio
lakini ghafla wananchi wakaibua hamasa kubwa ya 9 Dei ambayo ilishambihiana na ile
ya 19 Dei.
Katika siku hii ya kihistoria ya tarehe
19 Dei 1356 mwaka wa Kiirani, iliyosadifiana na tarehe 9 Januari, 1978,
kuliibuka harakati ya Chuo cha Kidini (Hawza) cha Qum ya kupinga kuchapishwa
makala iliyomvunjia heshima Imam Khomeini MA iliyochapishwa na gazeti la
Etelaat la nchini Iran. Maandamano ya kumpinga mtawala wa kiimla Shah Pahlavi
yalifanyika kote Iran wakati huo.