IQNA

Kiongozi Muadhamu aomboleza kifo cha Ayatullah Rafsanjani

11:59 - January 09, 2017
Habari ID: 3470790
IQNA-Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran, ametoa salamu za rambirambi kufuatia kufariki dunia Ayatullah Hashemi Rafsanjani.
Ofisi ya kuhifadhi na kusambaza turathi za Kiongozi Muadhamu imesambaza barua iliyoandikwa na Ayatullah Ali Khamenei kufuatia tukio hilo chungu. Katika barua hiyo Kiongozi Muadhamu sanjari na kuonyesha masikitiko yake makubwa kufuatia msiba huo, ametoa mkono wa pole kwa familia na watu wa karibu wa mwanazuoni huyo, mwanamapambano, alimu na mfuasi wa njia ya Imam Khomein (MA). Amesema na hapa ninamnukuu: "Kumkosa Ayatullah Ali Akbar Hashemi Rafsanjani simtambui mtu mwingine mwenye tajriba shirikishi na katika kipindi hiki kirefu nilichokuwa naye nitamkumbuka hasa katika kipindi cha milima na mabonde ya kihistoria.

Hivi sasa mwanamapambano huyu mkongwe yupo mbele ya Mwenyezi Mungu akiwa na faili lililojaa juhudi na harakati mbalimbali na hii ndio hatma ya viongozi wote wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran. Kwa moyo mkunjufu  ninamtakia maghfira, rehema na msamaha wa Mwenyezi Mungu na ninatoa pole kwa mke, watoto, ndugu na marafiki wake wote." Mwisho wa kunukuu. Kati ya nyadhifa ambazo Ayatullah Rafsanjani aliwahi kuzishika baada ya ushindi wa mapinduzi ya Kiislamu ni pamoja na Rais wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, Mwenyekiti wa Baraza la Wataalamu wanaomchagua Kiongozi wa Mapinduzi ya Kiislamu, Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu (Bunge la Iran), Kaimu Amiri Jeshi Mkuu, Mwenyekiti wa Baraza Kuu la Ulinzi wa Kitaifa na nafasi aliyoishika hadi kifo chake ya Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kuainisha Maslahi ya Mfumo wa Kiislamu.

captcha