IQNA

Mahakama ya Ulaya yawalazimisha Wasichana Waislamu kuogelea pamoja na wavulana

15:25 - January 14, 2017
1
Habari ID: 3470794
IQNA: Mahakama ya Umoja wa Ulaya imetoa hukumu na kusema ni lazima wasichana Waislamu katika shule waogelee pamoja na wavulana.
Mahakama ya Ulaya yawalazimisha Wasichana Waislamu kuogelea pamoja na wavulana

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Mahakama ya Haki za Binadamu Ulaya (ECHR) Jumanne iliafiki hatua ya wakuu wa Switzerland kuwashurutisha watoto wa kike na kiume kushiriki pamoja katika masomo ya kuogele pamoja pasina kujadili itikadi zao za kidini.

Kesi hiyo ilikuwa imewasilishwa mahakamani na wanandoa raia wa Uswisi wenye asili ya Uturuki ambao walitaka mabanati zao Waislamu wasishurutishwe kushiriki katika masomo ya kuoglelea ambayo yanawajuuisha pia wanafunzi wa kiume.

Mahakama ya Ulaya imesema hatua ya wakuu wa Uswisi kuwashurutisha wasichana hao Waislamu kuoglelea pamoja na wanaume ni jambo ambalo linaingilia itikadi zao za kidini lakini ikahalalisha ushuritishaji huo kwa madai kuwa jambo hilo linawalinda watoto wasitengwe kijamii.

Mahakama hiyo imedai kuwa, "masomo ya kuogelea si kwa ajili ya kujifunza tu kuogelea bali ni kushiriki katika harakati ya pamoja na wanafunzi wengine."

Halikadhalika mahakama hiyo ya Ulaya imesema wazazi wanaowazuia watoto wao kushiriki katika masomo ya kuogelea watozwe faini ya $ 1,380 ili kuhakikisha kuwa wazazi wote wanawatuma watoto katika masomo ya kuogelea. Hii si mara ya kwanza Uswisi kupitisha sheria tata zenye kuwapokonya Waislamu haki zao.

Mwezi Mei mwaka jana pia mamlaka za kieneo za Uswisi zilipitisha kanuni ya kuwashurutisha wanafunzi Waislamu kuwaamkua kwa mkono walimu wao ambao sio wa jinsia zao, la sivyo watozwe faini ya dola 5,000 za Marekani.

Kanuni hiyo imetengua mwongozo uliokuwa umetolewa na shule moja ya manispaa ya Therwil katika wilaya ya Arlesheim nchini humo, wa kukubali ombi la wanafunzi wawili wa Kiislamu wa kiume kutowapa mkono wanafunzi na walimu wa kike, kama wanavyofunzwa na dini yao tukufu ya Kiislamu.

Wanafunzi hao ni watoto wa Imamu wa Msikiti mmoja katika mji wa Basel, raia wa Syria aliyepewa hifadhi na Usiwisi mwaka 2001.

Mwaka 2009 pia Uswisi ilipiga marufu ujenzi wa minara katika misikiti ya nchi hiyo na kuitaja kuwa nembo ya Uislamu inayoharibu mandhari ya nchi hiyo ya Ulaya.

iqna.ir/en/news/3461915

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Swalehe Mdungu
0
0
waislam tuamken tusikubali kudhulumiwa haki zetu
captcha