IQNA

Msikiti wateketezwa moto Washington, Marekani

14:52 - January 15, 2017
Habari ID: 3470797
IQNA: Watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wameuteketeza moto msikiti katika mji wa Bellevue, jimboni Washington nchini Marekani.
Msikiti wateketezwa moto Washington, Marekani

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, moto huo uliteketeza Kituo cha Kiislamu cha Eastside (ICOE) ambacho pia kinajulikana kama Bellevue Masjid au Bellevue Mosque mapema Jumamosi asubuhi. Kituo hicho cha Kiislamu kimekuwa kikiwahudumia Waislamu wa eneo hilo kwa muda wa miaka 14 sasa. Ingawa hakuna mtu yeyeote aliyejeruhiwa katika mtoto huo lakini nusu ya jengo hilo la Waislamu limeharibiwa kabisa katika moto huo.

Maafisa wa polisi wanasema wamemtia mbaroni mtu moja ambaye anashukiwa kuwasha moto huo huku uchunguzi ukiendelea kubaini kilichotumiwa kuteteketeza jengo hilo. Wakuu wa Bellevue Masjid wamewafahamisha Waislamu kuwa msikiti huo utafundw akwa muda na kwamba watakuwa wakisali katika kituo cha kijamii cha Highland Community Center.

Bellevue ndio mji wa tano kwa ukubwa katika jimbo la Washington na unakadiriw kuwa na idadi ya watu 135,000. Meya wa Bellevue ameutembelea msikiti huo na kulaani kitendo cha kuuteketeza moto huku akiwahakikishia Waislamu kuwa yuko nao katika kipindi hiki cha masaibu.

Kumeshuhudiwa wimbi la hujuma dhidi ya Waislamu kote Marekani baada ya Donald Trump kutangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa rais.

Kwa mujibu Baraza la Mahusiano ya Kiislamu na Marekani (CAIR), ambalo hutetea haki za Waislamu, mbali na misikiti na vituo vya Kiislamu kushambuliwa pia wanawake na watoto Waislamu wamekuwa wakishambuliwa mara kwa mara na watu wenye chuki dhidi ya Uislamu.

http://iqna.ir/fa/news/3562743

captcha