Ibrahim Mussa ameeleza kuwa, nyaraka zilizofichuliwa na duru za kuaminika na ambazo ziko karibu na mashirika ya kijasusi ya nchi hiyo zinaonesha kuwa, baadhi ya mamluki wa ndani na wa nje wanafanya njama za kukiuka amri ya mahakama inayotaka kuachiliwa huru Sheikh Zakzaky.
Kwingineko, Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye anashikiliwa katika jela ya Nigeria ametoa ujumbe akisema hana wasiwasi kuhusu kuendelea kushikiliwa jela au kuachiwa huru, kwa sababu Mwenyezi Mungu Muweza huwatunuku kheri waja wake popote pale walipo.Sheikh Ibrahim Zakzaky akiwa na mke wake alitiwa mbaroni na Jeshi la Nigeria mwezi Disemba mwaka 2015 katika kituo cha kidini huko katika mji wa Zaria kaskazini mwa jimbo la Kaduna. Tokea wakati huo Sheikh Zakzaky na mkewe wamekuwa wakizuiliwa katika mojawapo ya vituo vya kijeshi vya nchi hiyo bila kufunguliwa mashktaka.
Jeshi hilo lilidai kuwa wafuasi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria walikuwa na njama ya kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Nigeria, madai ambayo yamekanushwa vikali na wafuasi wa harakati hiyo.
Jeshi hilo katili liliizika miili ya waliouawa katika kaburi moja kwa lengo la kuficha ushahidi wa ukubwa wa jinai hiyo. Inakadiriwa kuwa Waislamu 1000 wasio na hatia waliuawa katika tukio hilo huku Sheikh Zakzaky, ambaye hali yake ya kiafya si nzuri, akiendelea kushikiliwa korokoroni pasina kufunguliwa mashtaka.