IQNA

Trump alaaniwa kwa kuwapiga marufuku Waislamu kuingia Marekani

11:27 - January 28, 2017
Habari ID: 3470817
IQNA-Rais Donald Trump wa Marekani amelaaniwa vikali kwa hatua yake ya kutia saini sheria ya kuwapiga marufuku Waislamu kuingia nchini humo.
Trump alaaniwa kwa kuwapiga amrufuku Waislamu kuingia Marekani

Marekani ametia saini amri ya kuwazuia Waislamu kuingia nchini humo ambapo hivi sasa kutakuwa na vizingiti kwa wahamiaji na wakimbizi kwa lengo la kuwazuia watu aliowataja kuwa, 'magaidi wa Kiislamu wenye misimamo mikali' kuingia katika nchi hiyo.

Akizungumza Ijumaa baada ya kutia saini amri hiyo inayoonyesha uhasama na chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu, Trump alitaja utiwaji saini sheria hiyo kuwa hatua kubwa ingawa hakutoa maelezo zaidi kuhusu yaliyomo.

Rasimu iliyovuja ya sheria hiyo inaonyesha kuwa, wakimbizi kutoka Syria watazuiwa kuingia Marekani huku wahajiri kutoka nchi za Waislamu kama vile Sudan, Somalia, Iraq, Iran, Libya na Yemen wakipigwa marufuku kwa muda kuingia Marekani.

Wakati wa kampeni zake, Trump alikuwa ametaka Waislamu wazuiwe kikamilifu kuingia Marekani huku kukiwa na taarifa kuwa, rais huyo wa ameanza kutekeleza mpango wa kuwasajili Waislamu wote Marekani kwa lengo la kudhibiti nyendo zao.

Seneta Elizabeth Warren wa Massachusetts amemlaani vikali rump kwa amri yake hiyo ya kuwazuia Waislamu wa baadhi ya nchi za Kiislamu kuingia Marekani. "Hatua ya Trump ya kuwawekea vizingiti vikali wahamiaji kutoka nchi za Kiislamu na kupiga marufuku wakimbizi ni jambo ambalo linakiuka thamani za Kimarekani." Amesema Marekani ni nchi ambayo imejengwa na wakimbizi, wahamiaji na watu wengine ambao waliingia nchini humo wakikimbia ukandamizaji katika nchi zao. Aidha seneta wa Kamal Harris naye pia amemlaani vikali Trump kwa kuwauzi Waislamu kuingia nhcini humo na kusema kimsingi rais huyo amewapiga marufuku Waislamu kuingia Marekani.

http://iqna.ir/en/news/3462054

Kishikizo: trump waislamu
captcha