IQNA

Rais wa Gambia asema nchi yake si Jamhuri ya Kiislamu tena

19:21 - January 29, 2017
2
Habari ID: 3470819
IQNA-Rais mpya wa Gambia ametangaza kuwa nchi yake haitajulikana tena kama Jamhuri ya Kiislamu ya Gambia ikiwa ni katika kutekeleza ahadi ya kampeni zake za uchaguzi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika amri aliyoitoa Jumamosi 28, Januari, Rais Adama Barrow wa Gambia alisema jina rasmi la nchi hiyo halitakuwa tena na sifa ya 'Kiislamu'. Mnamo mwaka 2015 Rais wa zamani wa Gambia Yahya Jammeh aliitangaza nchi hiyo ya magharibi mwa Afrika kuwa Jamhuri ya Kiislamu baada ya kujiondoa katika Jumuiya ya Madola mwaka 2013.

Barrow amebaye ameingia madarakani kufuatia mashinikizo ya nchi za Magharibi amesema nchi hiyo, ambayo asilimi 90 ya watu wake ni Waislamu, haitajulikana tena kama Jamhuri ya Kiislamu.

Barrow alirejea Gambia Alhamisi baada yakuondoka mtangulizi wake aliyeiongoza nchi hiyo ndogo ya magharibi mwa Afrika kwa miaka 22, Yahya Jammeh. Barrow ambaye ni Mwislamu, aliishi Uingereza kwa muda mrefu kabla ya kurejea Gambia mwaka 2006 na kuingia katika siasa.

Jammeh ambaye sasa yuko uhamishoni nchini Equatorial Guinea, alikuwa amekubali kushindwa na Barrow katika uchaguzi wa rais uliofanyika mwezi Desemba na hata kumpongeza mpinzani wake huyo lakini ghafla alibadilisha uamuzi na kuyakataa matokeo kwa madai kuwa zoezi la uchaguzi lilitawaliwa na dosari nyingi na sasa anataka uchaguzi wa rais ufanyiketena.

Jammeh alikubali kuondoka madarakani wiki iliyopita baada ya nchi za Magharibi mwa Afrika kutisha kutuma majeshi nchini humo kumuondoa madarakani kwa nguvu.

3567970/

Imechapishwa: 2
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Bila jina
0
0
Yote ni mipango ya Allah.
Balinda
0
0
Uingereza hakutoke wazima, hata wenye kuaribu uislamu na waislamu BARA ARAB walitoka ungereza london. najo wenye ku uaribu umoja wakiislamu.
hata #rais wa gambia akatale nchi iyo kubaki ya kiislamu hataweza kubadili mushimamo ya waislamu.
captcha