IQNA

Umoja wa Mataifa

Kuna mauaji ya kimbari ya Waislamu nchini Myanmar

18:23 - February 03, 2017
Habari ID: 3470831
IQNA-Umoja wa Mataifa umesema mamia ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa nchini Myanmar katika ukandamizaji wa miezi ya hivi karibuni katika kile kinachoonekana ni mauaji ya kimbari.

Ripoti ya Ofisi ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa imesema mamia ya Waislamu wa kabila la Rohingya wameuawa nchini Myanmar katika ukandamizaji wa miezi ya hivi karibuni katika kile kinachoonekana ni mauaji ya kimbari.

Katika taarifa iliyotoelewa Ijumaa, Zeid bin Ra’ad al-Hussein Kamishna wa Haki za Binadamu aktika Umoja wa Mataifa amesema vikosi vya usalama Myanmar vimetekeleza mauaji ya umati, ubakaji wa Waislamu kigenge na kuteketezwa vijiji vyao katika kampeni mpya ya ukandamizaji iliyoanza mwezi Okotba mwaka jana.

Wakaguzi wa Umoja wa Mataifa wamerekodi vitendo vipya ya ukatili ikiwa ni pamoja na mateso, utekaji nyara, ubakakji wa kigenge na mmauaji ya watoto wachanga, kwa mfano miezi minane, mikononi mwa jeshi la Myanmar.

"Serikali ya Myanmar inapaswa kusitisha amra moja ukiukwaji huu mkubwa wa haki za binadamu za raia wake," amesema Hussein.

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa ametangaza ripoti hiyo baada ya Myanmar kuzuia maafisa wa umoja huo kuingia jimbo la Rakhine ambalo ni makao ya Waislamu wa kabila la Rohingya.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Umoja wa Mataifa, Waislamu wa Rohingya 65,000 ambao wamekimbia mchafuko ya hivi karibuni huko Myanmar, hivi sasa wanaishi kambini huko Bangladesh.

Halikadhalika Mabudha wanaounda asilimia 53 ya jamii yote ya nchi hiyo wamekuwa wakihusika na mauaji dhidi ya Waislamu wa kabila la Rohingya katika mkoa wa Rakhine. Ukandamizaji huo ulishika kasi mwaka 2012 ambapo Mabudha hao wakisaidiwa na maafisa usalama wa Myanmar wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali za ukatili, mauaji na hata kubaka wanawake Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo, mbali na kunyimwa uraia Waislamu wa jamii ya Rohingya wapatao milioni 1.1. Umoja wa Mataifa umewataja Waislamu wa Myanmar kuwa jamii iliyokandamizwa zaidi dunaini.

Hivi karibuni, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetoa wito kwa nchi za Kiislamu kuwasaidia Waislamu wa kabila la Rohingya nchiniMyanmar wanaokabiliwa na mateso. Kauli hiyo ilitolewa na Waziri wa mambo ya nje ya Iran ambaye pia amekosoa kimya cha jamii ya kimataifa kuhusu kukandamizwa Waislamu hao wa Myanmar.

Zarif alitoa kauli hiyo katika kikao maalumu cha mawaziri wa mambo ya nje wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC huko, Kuala Lumpur Malaysia.

3570071


captcha