IQNA

Tanzania yatangaza wawakilishi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Iran

14:12 - February 12, 2017
Habari ID: 3470845
IQNA: Mashindano ya Qur'ani yamefanyika nchini Tanzania wiki hii kuchagua wawakilishi wa nchi hiyo ya Afrika Mashariki katika mashindano yajayo ya kimataifa katika Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Ofisi ya Mwambata wa Utamaduni wa Iran nchini Tanzania imeandaa mashindano hayo ambayo yalifanyika Februari 9-11 kwa ushirikiano wa Taasisi wa al-Istiqama.

Washiriki kutoka kote Tanzania walishindana katika vitengo vya kusoma na kuhifadhi Qur'ani kwa lengo la kupata nafasi ya kushiriki katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran. Mashindano hayo ya Qur'ani nchini Tanzania yalianza Alhamisi na kumalizika Jumamosi na yamefanyika pia kwa munasaba wa maadhimisho ya mwaka wa 38 wa ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu ya Iran.

Kati ya wageni wa heshima waliohudhuria mashindano hayo yaliyofanyika mjini Dar es Salaam ni makamu wa zamani wa rais wa Tanzania Dkt. Gharib Bilal, Balozi wa Iran nchini Tanzania Bw. Musa Farhang na mwambata wa utamaduni wa Iran nchini Tanzania Bw. Ali Bagheri.

Washindi katika mashindano hayo walikuwa Abdul Hamid Masoud ambaye ataiwakilisha Tanzania katika kategoria ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu na Adam Juma ambaye ataiwakilisha nchi yake katika kitengo cha qiraa au kusoma Qur'ani.

Katika kitengo cha wanawake, Arifah bint Hussen na Suria Ali wataiwakilisha Tanzania katika kuhifadhi Qur'ani kikamilifu na qiraa kwa taratibu.

Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'ani ya Iran yamepangwa kufanyika mjini Tehran baadaye mjini Aprili.

3573496

captcha