IQNA

Makundi yanayowapinga Waislamu yaongezeka mara tatu Marekani baada ya Trump

18:32 - February 17, 2017
Habari ID: 3470853
IQNA-Idadi ya makundi yanayowapinga Waislamu yammeongezeka karibu mara tatu Marekani mwaka 2016 baada ya kuanza kampeni za urais za Donald Trump.

Kwa mujibu wa ripoti, mwaka 2015 kulikuwa na makundi 34 yaliyo dhidi ya Waislamu Marekani lakini makundi hayo yaliongezeka na kufika 101 mwaka 2016.

Shirika la Southern Povert Law Centre (SPLC) limefanya uchunguzi na kubaini kuwa matamshi ya chuki dhidi ya Waislamu ya Trump wakati akigombea urais ndio chanzo kikuu cha kuongezeka chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Marekani.

Uchunguzi huo ambayo umefanywa na umebaini kuwa, mwaka 2016 ulivunja rekodi Marekani kwa kiwango cha chuki dhidi ya Waislamu.

Shirika hilo limesema kwa ujumla kuna makundi zaidi ya 900 yenye kueneza chuki dhidi ya kaumu zinginezo kote Markeani. Makundi hayo yanajumuisha pia yale ya wazungungu wanazi wenye misimamo mikali ya kibaguzi na pia makundi ya Wamarekani wenye asili ya Afrika ambao wanataka kujitenga na Marekani.

Shirika hilo limesema kuibuka Trump ghafla mwaka 2016 katika kampeni za uchaguzi wa rais ni jambo ambalo lilichangia kiasi kikubwa kuongezeka wimbi la makundi ya kibaguzi na yenye chuki ambayo yalikuwa hayajitokezi hadharini kwa miongo mingi katika jamii ya Marekani.

Baada ya ushindi wa Trump na kuapishwa kwake Januari 20 kumeshuhudiwa hujuma dhidi ya misikiti na vituo vya Kiislamu Marekani na pia katika nchi jirani ya Canada.

Mwezi moja baada ya ushindi wa Trump katika uchaguzi wa Novemba 8, Shirika la SPLC linasema liliweza kurekodi vitendo 1,098 vya chuki kote Marekani ambapo idadi kubwa ya waliotekeleza vitendo hivyo walimtaja Trump na nara yake ya Kuifanya Marekani Kuwa na Nguvu Tena (Make America Great Again) au matamshi yake dhidi ya wanawake.

3575142

captcha