IQNA

Washindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Iran wazawadiwa

18:51 - February 18, 2017
Habari ID: 3470855
IQNA: Washindi wa Mashindano ya Kitaifa ya Qur'ani Tukufu nchini Iran wametunukiwa zawadi katika hafla iliyofanyika mjini Tehran Ijumaa.

Mashindano hayo ambayo yaliandaliwa na Kituo cha Darul Qur'an cha Imam Ali (AS) yalifanyka katika Ukumbi wa Mashahidi wa Mapinduzi ya Kiislamu na kufungwa katika sherehe iliyohudhuriwa na maulamaa, maafisa wa utamaduni na wanaharakati wa Qur'ani.

Sherehe hizo zilianza kwa qiraa ya Qur'ani Tukufu na kisha ujumbe wa Ayatullah Jafar Subhani ambayo alisisitiza kuhusu thawabu za mwenye kuhudumia Qur'ani Tukufu.

Mkuu wa Kituo cha Darul Qur'an cha Imam Ali (AS), Mohammad Ansari aiwasilisah ripoti kuhusu mashindano hayo na kusema watu 2700 walishiriki ambapo 1310 waliingia fainali.

Naye Mehdi Qarasheikhlu, mkurugenzi wa Shirika la Darul Qur'an Karim la Iran amesema majaji katika mashindano hayo walikuwa miongoni mwa maustadhi bingwa wa Qur'ani nchini Iran. Washindi wa kategoria tatu za mashindano hayo walitunukiwa zawadi.

Duru ya 10 ya mashindano ya kitaifa ya Qur'ani ilianza Jumatatu, Februari 13 hadi Ijumaa.

3462231
captcha