IQNA

Qur'ani Tukufu, kitabu kilichouzwa kwa wingi maonyesho ya vitabu Morocco

20:20 - February 19, 2017
Habari ID: 3470857
IQNA: Qur'ani Tukufu ndicho kitabu kilichouzwa kwa wingi katika Maonyesho ya Kimataifa ya Vitabu, Casablanca, Morocco.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Bw. Fouad Mkurugenzi wa Kituo cha Kuchapisha na Kusambaza Vitabu Morocco, ambacho kimeandaa maonyesho ya mwaka huu, idadi ya nakala za Qur'ani tukufu zinazonunuliwa katika maonyesho hayo huongezeka kila mwaka.

Amesema vitabu vya hadithi na vitabu vya kujiboresha kimaisha ni kati ya vitbau ambavyo pia vilinunuliw akwa wingi katika maonyesho hayo.

Maonyesho ya 23 ya Kimataifa ya Vitabu Casablanca yalianza Februari 9-19 na kuhudhuriwa na wachapishaji 700 kutoka nchi 24.

Waziri wa Utamaduni wa Morocco, Mohamed Amin Sbihi amesema maonyesho hayo ni kati ya maonyesho muhimu zaidi duniani. Aidha amesema maonyesho ya mwaka huu yalikuwa na nchi 11 za kaskazini mwa Afrika ambazo zilipokea mwaliko maalumu.

3575870
captcha