IQNA

Kiongozi wa Hizbullah aipongeza Iran kwa kuunga mkono harakati za Palestina

10:00 - February 21, 2017
Habari ID: 3470861
IQNA: Kiongozi wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Lebanon ameipongeza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa kuendelea kuunga mkono Palestina wakati nchi zingine zimeegemea upande wa utawala haramu wa Israel.
Hivi karibuni Rais Trump wa Marekani alisema nchi yake haituanga mkono suluhisho hilo la nchi mbili. Sayyed Nasrallah amesema hatua hiyo ya Marekani ni muhimu kwani imehitimisha hadaa ya Israel kwa Wapalestina na kusema hivi sasa malengo halisi ya utawala wa Tel Aviv yatabainika. Kuhusu vitisho vya hujuma ya kijeshi dhidi ya Iran, Sayyed Nasrallah amesema vitisho hivyo ni vita vya kisaikolojia kuishinikiza Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ilegeze misimamo yake ya msingi. Amesema hivi sasa Marekani haina uwezo wa kuanzisha vita dhidi ya Iran kwani inafahamu kuwa Iran haitakuwa peke yake katika vita hivyo.

Katika mahojiano maalumu na Kanali ya Kwanza ya Shirika la Utangazaji la Iran IRIB yaliyorushwa hewani Jumatatu usiku, Nasrallah amesisitiza kuwa, Iran inatuma ujumbe mzito wa mshikamano na Palestina kwa kuandaa Kongamano la Kimataifa la Kuunga Mkono Intifada (mwamko) ya Palestina.

Mkutano wa kimataifa wa siku mbili kuhusu kuunga mkono mwamko wa Palestina unaanza leo hapa mjini Tehran kwa kuhudhuriwa na washiriki kutoka nchi 80. Sayyed Nasrallah amesema mkutano huo unafanyika katika wakati muhimu wa mabadiliko ya sera za Marekani kuhusu kile kinachotajwa kuwa suluhisho la nchi mbili baina ya Palestina na Israel. 

3462260/

captcha