IQNA

Imamu wa msikiti apigwa risasi na kuuawa mjini Baghdad

22:19 - March 03, 2017
Habari ID: 3470877
IQNA-Imamu wa msikiti mmoja katika mji mkuu wa Iraq, Baghdad amepigwa risasi na kuuawa magharibi mwa mji huo.

Kwa mujibu mwa mwandishi wa IQNA, duru za usalama Iraq zinadokeza kuwa, mtu mmoja asiyejulikana aliyekuwa na bunduki iliyopozwa sauti (silencer) , huku akiendesha pikiki alimpiga risasi na kumuua Sheikh Abdulsalam Al Hudaithi Alhamisi usiku. Sheikh Al Hudhaithi alikuwa Imamu wa Msikti wa Chuo Kikuu cha Al Akhawat Aswalihin katika eneo la Al Amiriya mjini Baghdad na alipigwa risasi karibu na nyumba yake.

Maafisa wa usalama nchini Iraq wameanzisha uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanazuoni huyo wa Kiislamu

Kwa mujibu mwa mwandishi wa IQNA, duru za usalama Iraq zinadokeza kuwa, mtu mmoja asiyejulikana aliyekuwa na bunduki iliyopozwa sauti (silencer) , huku akiendesha pikiki alimpiga risasi na kumuua Sheikh Abdulsalam Al Hudaithi Alhamisi usiku. Sheikh Al Hudhaithi alikuwa Imamu wa Msikti wa Al Ikhwat Salihin katika eneo la Awamiya mjini Baghada na alipigwa risasi karibu na nyumba yake..

Maafisa wa usalama nchini Iraq wameanzisha uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanazuoni huyo wa Kiislamu.Imamu wa msikiti apigwa risasi na kuuawa mjini Baghdad

Hivi karibuni Umoja wa Mataifa ulisema takriban raia elfu 7 wameuawa katika mapigano na mashambulizi ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh au ISIS mwaka uliomalizika wa 2016 nchini Iraq.

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Iraq(UNAMI) ulisema kuwa, raia6,878 wameuawa kutokana na mashambulizi na jinai za kutisha za ISIS katika nchi hiyo ya Kiarabu mwaka 2016 pekee. Taarifa ya UNAMI imeongeza kuwa, raia wengine12,388 wamejeruhiwa katika hujuma na jinai hizo za ISIS na makundi mengine ya kigaidi mwaka uliomalizika.

3580148
captcha