IQNA

Wanafunzi Waislamu Ujerumani waziuwa kuswali Shuleni

14:03 - March 04, 2017
Habari ID: 3470878
IQNA-Wanafunzi Waislamu katika shule moja Ujerumani wamepigwa marufuku kutekeleza ibada ya Swala wakiwa shuleni
Wanafunzi Waislamu Ujerumani waziuwa kuswali Shuleni

Barua ya uongozi wa shule hiyo iliyoko katika mji wa Wuppertal kwa walimu wa shule inawataka walimu hao kuwaripoti kwa uongozi wa shule wanafunzi Waislamu watakaoonekana wakiswali shuleni hapo.

Sehemu nyingine ya barua hiyo inasema kuwa, katika majuma ya hivi karibuni kumeshuhudiwa wanafunzi Waislamu shuleni hapo wakichukua udhu hadharani, wakitandika miswala na kisha kuswali, vitendo ambavyo wakuu wa shule wamedai kuwa eti ni uchochezi

Kwa mujibu wa agizo hilo, wafanyakazi na walimu wametakiwa kuwatafuta wanafunzi hao wanaotekeleza ibada ya Swala shuleni na kuwaripoti kwa uongozi ili hatua za kinidhamu zichukuliwe dhidi yao.

Aidha hatua ya awali inataka kuwapatia nasaha wanafunzi Waislamu kwamba, kitendo chao cha kuswali shuleni ni kinyume na sheria kwani ni marufuku kuswali shuleni.

Viongozi wa serikali ya Ujerumani wanadai kwamba, hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuwa, baadhi ya walimu na wanfunzi wasiokuwa wa Kiislamu wamekuwa wakikereka na hatua ya wanafunzi hao kuchukua udhu hadharani na kuswali. Aidha taarifa hiyo imeendelea kudai kwamba, marufuku hiyo imechukuliwa ili kushajiisha suala la kuishi pamoja na kupatikana uhakika wa amani shuleni. Waislamu nchini Ujerumani wamekuwa wakikabiliwa na wimbi la chuki dhidi ya Uislamu kutoka pande zote.

Mwezi Januari Kansela Angela Merkel wa Ujerumani katika kikao cha chama chake cha Wademokrat Wakristo alisema niqabu inayovaliwa na wanawake Waislamu inapaswa kupigwa marufuku katika maeneo ya umma.

Vazi la niqabu ni aina ya Hijabu ambayo huvaliwa na baadhi ya wanawake Waislamu huku wengi wakifadhilisha kuvaa Hijabu ambayo haifuniki uso kikamilifu

Hatua hiyo ya kuwapiga marufuku wanafunzi wa Kiislamu kuswali shuleni imelaaniwa vikali katika mitandao ya kijamii ambapo wengi wa walalamikaji wanasema, inakinzana wazi na madai ya nchi za Magharibi ya uhuru wa kuabudu.

3580141

captcha