IQNA

Vijana Waislamu Canada wapanga maonyesho 100 ya Qur'ani

16:21 - March 05, 2017
Habari ID: 3470880
IQNA-Jumuiya ya Vijana Waislamu huko Canada imepanga maonyesho 100 ya Qur'ani kote katika nchi hiyo katika kampeni ya 'Uislamu Ufahamike'.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, sambamba na maonesho hayo, vijana Waislamu watatemblea katika miji mbali mbali ya nchi hiyo katika fremu ya kuwafunza watu wa Canada kuhusu Uislamu.

Msemaji wa Jumuiya ya Vijana Waislamu Canada Imam Farhan Iqbal amesema, "Kwa kuzingatia mafundisho ya Kiislamu, tutajitahidi kuwafikia Wakanada wengi kadiri iwezekanavyo."

Ameongeza kuwa, "Tutaingia katika miji na kufika katika nyumba za watu huku tukizingumza nao kuhusu Uislamu."

Iqbal anasema kampeni hiyo inatoka na fikra potovu zilizopo kuhusu Uislamu jambo ambalo limepelekea kuongezeka wimbi dhidi ya Uislamu nchini humo na kote katika nchi za Magharibi.

Itakumbukwa kuwa Januari 30 mwaka huu, gaidi Mkristo aliwaua Waislamu sita katika msikiti mmoja nchini Canada. Gaidi huyo amebainika kuwa mfuasi wa Rais Donald Trump wa Marekani na alitumia bunduki aina ya AK47 aliwafyatulia risasi Waislamu waliokuwa katika msikiti wa Kituo cha Kiutamaduni cha Quebec, wakati wa Sala ya Ishaa.

3462332

captcha