IQNA

Wanajeshi wa Israel wamteka nyara mbunge mwanamke Mpalestina

10:27 - March 10, 2017
Habari ID: 3470888
IQNA: Wanajeshi wa utawala haramu wa Israel wamewateka nyara Wapalestina kadhaa akiwemo mbunge mwanamke katika oparesheni ya Alhamisi.

Mjumbe wa Bunge la Palestina Bi. Samira al Halayka ambaye ni mwanachama wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina, Hamas, alikamatwa akiwa nyumbani kwake katika mji wa al-Shoyoukh katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.

Duru zinadokeza kuwa mbunge huyo alifungwa pingu kisha akafunikwa macho na kupelekwa kusikojulikana na wanajeshi hao wa Israel.

Taarifa zinasema wanajeshi wa Israel pia walipora kompyuta yake na simu yake ya mkononi katika oparesheni hiyo ya utekaji nyara.

Baada ya kutekwa nyara al Halayka, idadi ywa wabunge wa Palestina wanaoshikiliwa katika korkoro za Israel imeongezeka na kufika 10.

Kwa ujumle kuna Wapalestina karibu 7,000 katika jela za kuogofya za utawala wa Kizayuni wa Israel.

Bunge la Palestina lenye wajumbe 132 linadhibitiwa na harakati ya Hamas na halijawahi kukutana tokea Juni 2007 wakati harakati hiyo ilipochaguliwa kuongoza Ukanda wa Ghaza.

3582378
captcha