IQNA

Mlipuko wa kigaidi karibu na Haram ya Bibi Sakina SA mjini Damascus

17:01 - March 11, 2017
Habari ID: 3470889
IQNA-Mabomu mawili yamelipuka katika mji mkuu wa Syria Damascus katika eneo lililo karibu na Haram ya Bibi Sakina SA na kupelekea wafanya ziara wasiopungua 45 kuuawa shahidi.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Idara ya Habari za Vita Syria imesema gaidi aliyekuwa amesheheni mada za milipuko alijiripua katika njia ya wafanyaziara waliokuwa wakielekea katika makaburi ya Bab al Saghir kuliko pia Haram ya Bibi Sakina SA mjini Damascus.

Baadhi ya duru zinasema hujuma hiyo ya kigaidi ilijumuisha mabomu mawili yaliyokuwa yametegwa ndani ya mabasi mawili yaliyokuwa yakitumiwa na wafanya ziara.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iraq Ahmad Jamal amelaani hujuma ya kigaidi na kusema Wairaqi 40 ni miongoni ya waliouawa wakati wakiwa katika ziara ya kidini.

Makaburi ya Bab al Saghir ni kati ya makaburi muhimu zaidi katika historia ya mji wa Damascus kwani ni sehemu ambayo wamezikwa baadhi ya watoto wa Maimamu 12 Watoharifu wa Waislamu wa Madhehebu ya Shia. Miongoni mwa waliozikwa hapo ni Bibi Sakina SA, bintiye Imam Hussein AS, mjukuu wa Mtume Muhammad AS. Halikadhalika katika makaburi hayo wamezikwa mashahaba watukufu wa Mtume SAW akiwemo Bilal Habashi AS. Bab al Saghir pia ni kati ya milango saba maarufu ya mji wa Damascus.

Hujuma hiyo ya kigaidi inaaminika kutekelezwa na magaidi wakufurishaji wa ISIS au Daesh ambao huwalenga Waislamu wa Madhehebu ya Shia na Sunni wasiokubaliana na itikadi zao potovu.

3582880

captcha