IQNA

Msikiti erevu kufunguliwa Imarati (UAE)

12:01 - March 15, 2017
1
Habari ID: 3470896
IQNA-Msikiti erevu (smart mosque) unatazamiwa kuzinduliwa kwa mara ya kwanza katika Umoja wa Falme za Kiarabu UAE.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, huku watu wengi UAE wakivutiwa na kila kitu ‘erevu’, msikiti wa kwanza ‘erevu’ na wa ‘kijani’ utafunguliwa katika la Ras Al Khaimah nchini humo.

Msikiti huo ambao umekuwepo kwa muda mrefu katika eneo laMuairidh sasa umekarabatiwa na uko tayari kutumika kwa kuzingatia teknolojia erevu na halikadhalika ni msikiti wa ‘kijani’kwa maana kuwa ujenzi wake umezingatia utunzwaji mazingira.

"Umeme wa vipaza sauti huwaka punde Imamu anaposimama juu ya zulia au msala katika mihrabu na huzimika wakati sala inapomalizika,” amesema Dkt. Hisham Al Refaei Al Mansuri msimamizi wa mradi huo.

Aidha anasema taa za msikiti huo zinatumia nishati ya jua na huwaka na kujizima zenyewe kwa kuzingatia wakati wa Sala na idadi ya waumini ndani ya msikiti. Dkt. Al Mansuri anaongeza kuwa, kiyoyozi au banka (air conditioner) katika msikiti huwaka na kuzimika sambamba na kubadlisha nyuzi joto kwa kuzingatia hali ya hewa na pia wa kutegemea idadi ya watu walio ndani ya msikiti.”

Hlikadhalika mifereji katika eneo la kutawadha (wudhuu) hutegemea sensa maalumu ili kuzuia israfu ya maji ambayo hushuhudiwa katika miskiti mingi duniani. Aidha maji yanayotumiwa kwa ajili wa wudhuu hutumiwa tena baada ya kusafishwa kwa mashine maalumu zilizohapo huku maji ya mvua nayo yakikusanywa kwa akiji ya kutumika kwa ajili ya mimea au bustani ya msikiti.

Msikiti huo ulikarabatiwa kwa msaada wa watu na mashirika ya kutoa misaada na inatazamiwa kuwa, kwa kutumia teknolojia hizo erevu na za kijani, msikiti huo utaweza kuokoa takribanidola 2,900 kila mwaka ambazo zingetumika kulipia umeme na maji.

Mradi huo umeungwa mkono na Jumuiya ya Dar al Ber na Jumuiya ya Misaada Sharjah kwa ushirikiano na Halmashauri ya Masuala ya Kiislamu na Waqfu nchini Imarati.

3584077

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Aidid Ali
0
0
mashaallah
captcha