IQNA

Mufti wa Misri: Imam Ali AS alitabiri kudhihiri ISIS

23:18 - April 15, 2017
1
Habari ID: 3470935
TEHRAN (IQNA)-Mufti Mkuu wa Misri Shawqi Ibrahim Abdel-Karim Allam amesema Imam Ali AS alitabiri kudhihiri kundi la kigaidi la ISIS zaidi ya miaka 1400 iliyopita.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Sheikh Shawqi Allam amesema karne 14 ziliopita Imam Ali alitabiri kwa njia sahihi kuhusu kuibuka kundi la magaidi wakufurishaji ambao wakati huo aliwataja kuwa, "Wenye bendera nyeusi". Mufti Shawki Allam ameashiria hadithi inayomnukulu Imam Ali AS akisema: "Wakati mtakapoona bendera nyeusi kaeni pale mlipo na tulizeni miguu na mikono yenu. Kutakuwa na watu wa kundi dhaifu ambao nyoyo zao zitakuwa ngumu kama chuma na watakuwa na dola lao. Wafuasi wa kundi hilo ni wakiukaji ahadi na huvunja mikataba. Watadai kuwa wenye haki lakini hawatakuwa na haki. Waitaitana kwa majina wa watoto wao na kwa lakabu za sehemu walikotoka. Watakuwa na nywele ndefu kama za wanawake na watahitilafiana baina yao wenyewe. Hali hii itaendepea hadi Allah atakapoleta haki kupitia atakayemtaka."

Mufti wa Misri amesema lengo la sheria za Kiislamu ni kulinda maisha ya mwanadamu katika hali ambayo nukta hiyo haiko katika kamusi ya magaidi wa ISIS au Daesh. Amesema ni kwa msingi huo ndio magaidi wakufurishaji wa ISIS wanatenda jina na kuwaua wanadamu kiholela katika hali ambayo Uislamu na dini zote zingine za mbinguni zinahimiza kulinda maisha na uhai. Amesema katika Uislamu hakuna mwenye haki ya kuchukua uhai wa mwanadamu mwingine isipokuwa kwa hukumu ya hakimu au katika zama za vita na wakati wa kujihami.Mufti wa Misri: Imam Ali AS alitabiri kudhihiri ISIS

Inafaa kuashiria hapa kuwa hadhithi ambayo Mufti Shawqi Allam ameinukulu na kuinasibisha na Imam Ali AS imetajwa na baadhi kuwa yenye isnad dhaifu huku baadhi ya wanazuoni wakiitaja kuwa sahihi na isiyo na dosari.

Utawala wa Saudi Arabia ambao uliasisisiwa na ukoo wa Aal Saud, katika ardhi iliyowahi kujulikana kama Hijaz, ni chimbuko halisi la fikra na idiolojia ya Kiwahhabi ambayo inatumiwa na makundi ya kigaidi ya Kitakfiri kama vile ISIS, Al Qaeda, Al Shabab, Taliban na Boko Haram. Makundi hayo yanachochea machafuko na oparesheni za kigaidi huko Syria, Iraq, Lebanon, Yemen, Pakistan, Libya, Somalia, Nigeria na maeneo mengine mengi duniani.

3589470
Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Yunus Yunus Ibrahim
0
0
Allah atulinde na ISIS
captcha