IQNA

Watanzania, Wamalawi na Warundi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Iran

10:36 - April 20, 2017
Habari ID: 3470942
TEHRAN (IQNA)-Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani ya Iran yana washiriki kutoka Tanzania, Malawi na Burundi wamewasili Tehran kuwakilisha nchi zao katika mashindano hayo.

Watanzania, Wamalawi na Warundi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani IranKatika taarifa kwa IQNA, Bw. Ali Baqeri Mwambata wa Utamaduni wa Iran mjini Dar es Salaam, Tanzania amesema ofisi yake imewateua wawakilishi kadhaa wa Tanzania, Malawi na Burundi kushiriki katika Mashindano ya 34 ya Kimatiafa ya Qur'ani Tukufu nchini Iran ambayo yameanza Jumatano mjini Tehran.

Wawakilishi wa Tanzania wameteuliwa kufuatia mashindano ya kitaifa ambayo hufanyika kila mwaka na hatimaye wenye kushika nafasi za kwanza huwakilisha nchi yao katika vitengo vya qiraa au kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu kikamilifu katika mashindano ya Tehran.

Kuna washiriki kadhaa kutoka Tanzania, Burundi na Malawi wanaowakilisha nchi zao katika mashindano ya kimataifa ya Qur'ani.

Wawakilishi wa Tanzania ni Bi. Thuraya Ali ambaye atashiriki katika mashindano ya wanawake ya kuhifadhi Qur'ani kikamilifu, Khamis Ali Pamba ambaye atashiriki katika mashindano ya kuhifadhi Qur'ani maalumu kwa wenye ulemavi wa macho, Adam Juma katika kitengo cha qiraa na tajwid na Abdul Masoud katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani kikamilifu. Wawakilisi wa Malawi ni Abdul Rashid Bili katika kitengo cha tajwid na qiraa katika mashindano ya kawaida huku Bilal Abdul Rashid akishiriki katika kitengo cha tajwid na qiraa katika mashindano maalumu ya wanafunzi wa vyuo vya kidini. Mwakilishi wa Burundi ni Ndugu Nduimana katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani kikamilifu.

Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran mwaka huu ni ya aina yake na ya kipekee duniani kwani ni mara ya kwanza kwa mashindano matano tafauti kufanyika wakati moja. Amesema mbali na yale ya kawaida ya wanaume kutakuwa pia na mashindano maalumu ya wanawake, watu wenye ulemavu wa macho, ya wanachuo wa vyuo vya dini na pia mashindano ya wanafunzi wa shule. Ameongeza kuwa, kauli mbiu ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iran ni "Kitabu Kimoja Umma Moja" na kuongeza kuwa mara hii imetokana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

3590874/


Watanzania, Wamalawi na Warundi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Iran

Watanzania, Wamalawi na Warundi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Iran

Watanzania, Wamalawi na Warundi katika Mashindano ya Kimataifa ya Qur'ani Iran
captcha