IQNA

Spika wa Bunge la Iran katika ufunguzi wa Mashindano ya Qur'ani

Baadhi ya nchi za Kiislamu zinashirikiana na Marekani, Israel kuwaua Waislamu

13:05 - April 20, 2017
Habari ID: 3470943
TEHRAN (IQNA)-Spika wa Majlisi ya Ushauri ya Kiislamu, Bunge la Iran, amesema ni jambo la kufedhehesha kwa baadhi ya nchi za Kiislamu zikishirikiana na Marekani na Israel kuwaua Waislamu.

Ali Jarijani aliyasema hayo Jumatano mjini Tehran alipohutubia ufunguzi wa Mashindano ya 34  ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran. Alisema machungu makubwa zaidi uliyonayo leo Ulimwengu wa Kiislamu ni ya hitilafu kati ya nchi za Kiislamu na kuongeza kuwa harakati za kuigaidi na ukufurishaji zinawadunisha Waislamu.

Dakta Larijani amebainisha kuwa kitendo cha makundi ya kigaidi cha kuzitumbukiza kwenye mgogoro nchi za Kiislamu kimeyafungulia njia ya kujiingizia kwenye nchi hizo madola ya nje ya eneo hili.

Huku akiashiria kwamba makundi hayo ya kigaidi na ukufurishaji yameupatia fursa ya kupumua utawala wa Kizayuni, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema baadhi ya nchi za Kiislamu zinahatarisha maisha ya Waislamu wa eneo hili kwa kuusaidia nyuma ya pazia utawala wa Kizayuni huku zikiuchukulia kuwa ni wa kirafiki uhamasishaji zinazopewa na Marekani na utawala wa Kizayuni.

Spika wa Bunge aidha amekosoa kuutumia ugaidi kimaslahi kunakofanya na madola ya Magharibi na kubainisha kuwa Magharibi inautumia vibaya uungaji mkono wa baadhi ya nchi za Magharibi kwa hatua za makundi ya kigaidi.

Dakta Larijani amesisitiza kuwa hakuna hoja ya kuhalalisha hitilafu, migogoro na mapigano kati ya nchi za Kiislamu.

Mashindano ya 34 ya kimataifa ya Qur'ani Tukufu yalifunguliwa rasmi jana hapa mjini Tehran yakihudhuriwa na washiriki 276 wa usomaji na kuhifadhi Qur'ani kutoka nchi 83. Mashindano hayo yanatazamiwa kuendelea hadi Jumanne tarehe 27 Rajab.

Mashindano ya 34 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu ya Iran mwaka huu ni ya aina yake na ya kipekee duniani kwani ni mara ya kwanza kwa mashindano matano tafauti kufanyika wakati moja. Amesema mbali na yale ya kawaida ya wanaume kutakuwa pia na mashindano maalumu ya wanawake, watu wenye ulemavu wa macho, ya wanachuo wa vyuo vya dini na pia mashindano ya wanafunzi wa shule. Ameongeza kuwa, kauli mbiu ya mashindano ya kimataifa ya Qur'ani nchini Iran ni "Kitabu Kimoja Umma Moja" na kuongeza kuwa mada hii imetokana na mafundisho ya Qur'ani Tukufu.

3591447

Spika wa Bunge la Iran katika ufunguzi wa Mashindano ya Qur'ani





captcha