Taarifa zinasema Wizara ya Elimu ya Madagascar imetumia kisingizio cha kukosekana suhula za kutosha kuwa sababu ya kufunga madrassa hizo za Qur'ani. Waziri wa Elimu katika nchi hiyo amezungumza kupitia radio ya taifa na kudai kuwa: "Taasisi hizi 16 awali zilianzisha kama madrassah binafsi za Kiislamu lakini hivi sasa zimegeuzwa na kuwa vituo vya kutoa mafunzo kamili na ya umma ya Qur'ani."
Amesema yuko tayari kukutana na wawakilishi wa Waislamu nchini humo ili kutoa ufafanuzi kuhusu uamuzi wake na kuongeza kuwa, uamuzi huo utaanza kutekelezwa baada ya kumalizika muhula huu wa masomo.
Uislamu umekuwepo nchini Madagascar hata kabla ya Ukristo kuanzia karne za 10 na 11 Miladia ambapo Waislamu wanakadiriwa kuwa takribani asilimia 10 ya watu wote milioni 24 katika nchi hiyo ambayo ni kisiwa kikubwa katika pwani ya kusini mashariki mwa Afrika. Uislamu uliingia Madagascar kupitia wahajiri kutoka nchi za bara Arabu na Zanzibar.
3596267