IQNA

Hofu yapelekea ufalme Bahrain kuahirisha hukumu ya Sheikh Qassim

19:24 - May 07, 2017
Habari ID: 3470971
TEHRAN (IQNA) Utawala wa kidikteta wa Aal-Khalifa nchini Bahrain, umeahirisha tena kesi ya Ayatullah Sheikh Isa Qassim.

Utawala wa ukoo Aal Khalifa Kiongozi umeakhirisha kesi hioyo kwa hofu ya kushindwa kudhibiti hali ya mambo nchini ikiwa utatoa hukumu dhidi yake.

Mahakama ya kifalme na kimaonyesho ya nchi hiyo leo Jumapili na kwa mara ya nne mtawalia, imeahirisha kesi hiyo hadi tarehe 21 ya mwezi huu. Hii ni katika hali ambayo, jana usiku Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini humo walivaa sanda kama ishara ya maandalizi kwa ajili ya kumtetea hadi kifo kiongozi huyo wa kidini. Sheikh Qassim anakabiliwa na shtaka la kukusanya khums ambayo kimsingi ni sehemu moja ya tano ya pato ambalo Waislamu wa madhehebu ya Shia hutoa kwa njia ya Mwenyezi Mungu SWT.

Uahirishaji wa kesi hiyo umejiri huku askari zaidi wa Saudia wakitumwa nchini Bahrain kwa lengo la kutekeleza ukandamizaji zaidi dhidi ya raia wa nchi hiyo, hasa baada ya kutangazwa hukumu tarajiwa dhidi ya Sheikh Isa Qassim. Inaelezwa kuwa, utawala huo wa kiditeta umehofia ghasia zinazoweza kuibuka katika kumtetea mwanazuoni huyo wa Kiislamu na kushika kasi zaidi harakati za mapinduzi. Tokea Juni mwaka jana wakati Sheikh Qassim alipopokonywa uraia wake, wakazi wa mji wa Diraz, wamekuwa wakikusanyika kuizingira nyumba ya mwanazuoni huyo mashuhuri ili kuonyesha uungaji mkono wao kwake dhidi ya uonevu na ukandamizaji wa utawala wa Aal Khalifa. Mnamo Juni 20, 2016, utawala wa waliowachache wa Aal Khalifa ulimpkonya Ayatollah Sheikh Qassim uraia wake na baada ya hapo kuvunja Taasisi ya Mafundisho ya Kiislamu iliyoasisiwa na mwanazuoni huyo.

Hivi karibuni Katibu Mkuu wa Chama cha Kiislamu cha Al Wifaq cha Bahrain Sheikh Ali Salman alinukuliwa akisema kuwa, kufikishwa kizimbani Ayatullah Sheikh Isa Qassim ni sawa na utawala wa Aal Khalifa kuwafikisha kizimbani na kuwalenga Waislamu wote wa madhehebu ya Shia nchini Bahrain. Sheikh Salman alitoa tamko hilo akiwa gerezani ambako amekuwa akitumikia kifungo tokea mwaka 2014 huku chama cha Kiislamu cha Al Wifaq nacho kikiwa kimepigwa marufuku na utawala wa Aal Khalifa.

Malalamiko na maandamano ya wananchi wa Bahrain dhidi ya watawala dhalimu wa nchi hiyo yamekuwa yakiendelea tokea tarehe 14 Februari 2011. Tokea mwanzoni mwa maandamano hayo watawala wa ukoo wa Aal Khalifa wamekuwa wakitekeleza mbinu tofauti za kupambana na wapinzani.

3596953

captcha