IQNA

Jumuiya Kubwa Zaidi ya Wafanyakazi Norway Kususia Israel

19:19 - May 13, 2017
Habari ID: 3470978
TEHRAN (IQNA)- Jumuiya kubwa zaidi ya wafanyakazi Norway imetangaza kususia bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel kulalamikia ukandamizaji unaofanya na utawala huo dhidi ya Wapalestina.

Jumuiya ya Mashirika ya Wafanyakazi Norway (LO) imepiga kura ya 197 kwa 117 kuunga mkono harakati ya kimataifa ya kususia Israel kiuchumi, kiutamaduni na kielimu.

Harakati ya Kimataifa ya Kususia Israel- Boycott, Divestment and Sanctions- (BDS), ambayo hutetea haki za Wapalestina, imepongeza hatua hiyo ya Wafanyakazi wa Norway na kusema ni njia muafaka ya kutetea haki za Wapalestina.

BDS imeitaka serikali ya Norway ishinikizwe kukata uhusiano wa kijeshi na Israel na kusitisha ushirikiano na mashirika yote yaliyo na uhusiano na utawala wa Kizayuni wa Israel. Hata hivyo waziri wa mambo ya nje wa Norway Borge Brende amekosoa hatua hiyo.

Harakati ya Kimatiafa ya Kususia Israel BDS ilianzishwa mwaka 2005 na mashirika zaidi ya 170 ya kutetea haki za Palesitna kwa lengo la kuishawishi jamii ya kimataifa iususie utawala wa Kizayuni wa Israel hadi utakapositisha ukandamizaji wa Wapalestina.

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni umezidi kutengwa kimataifa na hata sasa nchi za Ulaya zimejiunga na kampeni hiyo ya kuususia na kuutenga utawala huo dhalimu.

Sababu ya kutengwa utawala huo wa Kizayuni ni kutokana na kushadidi jinai zake na uporaji ardhi za Wapalestina.

Waliwmengu wametoa jibu lao kwa jinai za Israel dhidi ya Wapalestina kwa kushiriki katika maandamano dhidi ya utawala wa Kizayuni katika kila kona ya dunia hata katika nchi za Ulaya.

Katika miaka ya hivi karibuni, kila tarehe 6-18 mwezi Machi huadhimishwa Wiki ya Kupinga Utawala wa Ubaguzi wa Israel ambapo washiriki hujumuika pamoja na kulaani sera za kujitanua za utawala wa Kizayuni ambao msingi wake ni ubaguzi wa rangi, kaumu na dini. Utawala haramu wa Israel unafananishwa na utawala wa ubaguzi wa rangi (apartheid) ulioangushwa Afrika Kusini.

Wataalamu wa masuala ya Israel wanaamini kuwa utawala huo unapata hasara ya zaidi ya dola bilioni nane kwa mwaka kutokana na vikwazo na ususiwaji wa kimataifa. Taathira ya vikwazo hivyo inatazamiwa kuwa mbaya kutokana na azimio ambalo lilipitishwa mwezi Disemba dhidi ya Israel katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa lengo la kulaani ujenzi wa viteongji vya walowezi wa Kizayuni.

3462813

captcha