TEHRAN (IQNA)-Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu la Qatar liko Doha, mji mkuu wa nchi hiyo ya Ghuba ya Uajemi.
Jumba
hilo la makumbusho lina usanifu majengo uliopata ilhamu kutoka katika
usanifu majengo wa kale wa Kiislamu na lilifunguliwa Novemba 22 mwaka
2008. Jumba la Makumbusho la Sanaa za Kiislamu, Qatar linaonyesha sanaa
za Kiislamu kutoka mabara matatu.