Duru za kuaminika zinadokeza kuwa watu kadhaa
wameuawa shahidi hadi sasa tokea utawala wa Saudi Arabia uanzisha mzingrio
dhidi ya mtaa wa Al-Mosara katika mji wa Awamiyah.
Kuendelea mauaji dhidi ya Waislamu wa Kishia yanayofanywa na utawala wa Aal Saud kumezifanya jinai za familia hiyo zizidi kuonekana. Utawala wa familia yaAal Saud nchini Saudia badala ya kuchukua hatua zitakazopelekea kupunguza malalamiko na upinzani dhidi yake kwa kuwaridhisha wananchi, umeamua kutumia mkono wa chuma dhidi ya mrengo wa upinzani.
Katika miaka ya hivi karibuni utiaji mbaroni kiholela, mateso, ukandamizaji na kutolewa hukumu zisizo za kiadilifu ni mambo ambayo yameshuhudiwa yakiongezeka mno nchini Saudia, ambapo mauaji dhidi ya Mashia ni kilele cha ukatili wa utawala huo.
Kushadidi ukandamizaji dhidi ya Waislamu wa Kishia si tu kwamba, hakujawa na faida yoyote kwa utawala wa Riyadhbali kumeufanya mgogoro wa ndani nchini humo uzidi kutokota na kushika kasi. Baada ya Saudia kushadidisha vitendo vya ukandamizaji katika maeneo ya mashariki mwa nchi hiyo ambapo akthari ya wakazi wake ni Waislamu wa madhehebu ya Shia, kumeibuka malalamiko makubwa katika maeneo hayo na kupelekea kuzuka makabiliano baina ya vikosi vya usalama na raia wa kawaida.