Ridhwan Ma'ash Al-Jumuah, Katibu Mkuu wa Wizara ya Masuala ya Dini na Waqfu katika jimbo Ghardaia ameyasema hayo katika mkutano wa pili wa kitaifa wa Usomeshaji Qur'ani Tukufu ambao umefanyika kwa kaulimbiu ya "Mbinu za Usomeshaji Qur'ani; Malengo na Nyenzo".
Ma'ash Al-Jumua'h amebainisha kuwa hatua hiyo inachukuliwa kwa lengo la kuimarisha umoja wa kidini kwa ushirikiano wa wadau na wanaharakati wa masuala ya kidini.
Inafaa kuashiria hapa kuwa mkutano wa pili wa kitaifa wa Usomeshaji Qur'ani Tukufu umefanyika katika jimbo la Ghardaia lililoko kusini mwa Algeria kwa kuhudhuriwa na Mashekhe, Maimamu wa Sala ya Ijumaa na Wanaakademia wa Vyuo Vikuu kwa madhumuni ya kubuni mbinu na utaratibu wa aina moja wa usomeshaji Qur'ani Tukufu.
Washiriki wa mkutano huo wamehudhuria mafunzo ya amali na kubadilishana mawazo juu ya mustakabali wa usomeshaji Qur'ani na mbinu za kujadidisha usomeshaji huo kwa kufuata misingi ya kadiri na wastani.