IQNA

Mwakilishi wa Iran achukua nafasi ya pili mashindano ya Qur'ani Uturuki

14:08 - May 24, 2017
Habari ID: 3470992
TEHRAN (IQNA)- Sayyed Mostafa Husseini wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ametangazwa kushika nafasi ya pili katika qiraa katika Mashindano ya 5 ya Kimataifa ya Qur'ani Tukufu nchini Uturuki.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Husseini ametangazwa mshindi katika mashindano hayo yaliyoanza Ijumaa mjini Istanbul katika Msikiti wa Fatih.

Kulikuwa na washiriki 120 kutoka nchi 62 katika vitengo vya kusoma na kuhifadhi Qur'ani Tukufu. Baada ya awamu ya kwanza quraa 10 walifika katika fainali akiwemo Sayyed Mostafa Husseini wa Iran paoja na wawakilishi Tunisia, Philippines, Indonesia, Bangladesh, Yemen, Uturuki, Malaysia, Brunei, na Pakistan.

Washindi katika kitengo cha kuhifadhi Qur'ani watatangazwa baadaye. Mashindnao hayo ya Qur'ani huandaliwa kila mwaka na Idara ya Masuala ya Kidini (Diyanet) katika ofisi ya rais wa Uturuki.

3602845/

captcha