IQNA

Wizara ya Ulinzi ya Russia

Huenda kinara wa magaidi wa ISIS, al Baghdadi ameuawa Syria

12:42 - June 16, 2017
Habari ID: 3471020
TEHRAN (IQNA)-Russia imetangaza kuwa inachunguza ripoti zinazoashiria kuwa huenda kinara wa kundi la kigaidi la ISIS au Daesh, Abu Bakr Al-Baghdadi ameuawa katika hujuma ya ndege za Russia nchini Syria.

Katika taarifa Wizara ya Ulinzi ya Russia, imesema, mnamo Mei 28, ndege za kivita za Russia za Su-34 na Su-35 zilitekeleza mashambulizi karibu na ngome ya ISIS mjini Raqqa kaskazini mwa Syria.

Taarifa zinasema zinasema miongoni mwa waliokuwa katika mkutano wa makamanda wa ISIS walilolengwa ni kinara wa ISIS al-Baghdadi.

Aidha mkutano huo ulikuwa na magaidi 300 ambao walikuwa na jukumu la kuwalinda makamanda hao wa ISIS aliokadiriwa kuwa 40 akiwemo al Baghdadi.

Taarifa hiyo imesema: "Kwa mujibu wa ripoti kadhaa, kiongozi wa ISIS Ibrahim Abu Bakr al-Baghdadi, ambaye aliuwawa katika hujuma hiyo ya ndege, alikuwa katika mkutano huo.

3610127

captcha