IQNA

Waislamu CAR katika hali mbaya Mwezi wa Ramadhani, wanasakamwa na Anti-Balaka

11:22 - June 20, 2017
Habari ID: 3471027
TEHRAN (IQNA) Waislamu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati wanakabaliwa na hali mbaya huku wengi wakiwa hawana chakala wala makao katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani baada ya kufurushwa na genge la Kikristo la Anti Balaka.

Taarifa zinasema maelfu ya Waislamu walikimbia makazi yao mwezi Mei kufuatia mapigano makali katika mji wa Bangassou mashariki mwa nchi hiyo.

Mgogoro wa sasa mjini humo ulianza baina ya Mei 13-17 wakati genge la kigaidi la Anti-Balaka ambalo aghalabu ya wafuasi wake ni Wakristo walipoanzisha hujuma dhidi ya mtaa wa Tokoyo ambao wakaazi wake wengi ni Waislamu. Kufuatia hujuma, hiyo maelfu ya Waislamu waliazimika kukimbilia hifadhi ndani ya msikiti wa eneo hilo. Hatahivyo msikiti haukuwa salama kwani magaidi wa Anti-Balaka waliuvamia na kumuua Imamu wa hapo na hivyo kuwalazimu Waislamu kutafuta hifadhi katika kanisa kuu mjini humo.

Waislamu wanaendelea kuhujumiwa na kuuawa mjini Bangassou pamoja na kuwa kuna askari wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa mjini humo maarufu kama MINUSCA. Aidha wanajeshi wa serikali ya nchi hiyo hawajatoa ulinzi wowote kwa Waislamu wanaoendelea kukandamizwa kote Jamhuri ya Afrika ya Kati. Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa wakaazi wapatao 35,000 wa Bangassou walikimbilia nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kufuatia mapigano mapya yaliyoibuka nchini humo mwezi Mei.Waislamu CAR katika hali mbaya Mwezi wa Ramadhani, wanasakamwa na Anti-Balaka

Jamhuri ya Afrika ya Kati ilitumbukia katika mgogoro na machafuko, mwaka 2013 baada ya kuzuka mapigano ya kidini na kikaumu yaliyopelekea kuondolewa madarakani serikali ya Rais François Bozizé. Genge la Kikristo la Anti-Balaka linatuhumiwa kutenda jinai dhidi ya raia wa nchi hiyo hasa Waislamu.

3610738

captcha