IQNA

Jeshi la Polisi Marekani ladai mauaji ya binti Mwislamu si ya kigaidi

14:48 - June 20, 2017
Habari ID: 3471028
TEHRAN (IQNA)-Katika hatua inayoatathminiwa kuwa ya kibaguzi, Jeshi la Polisi nchini Marekani limedai mauaji ya binti Mwislamu nje ya msikiti si ya kigaidi.

Binti huyo Mwislamu aliyetambuliwa ka jina la Nabra Hassanen,aliuawa Jumapili iliyopita baada ya kutoka msikitini katika jimbo hilo ambapo alitekwa nyara na kupigwa na mtu mwenye chuki dhidi ya Uislamu katika jimbo la Virginia.

Polisi imetangaza kuwa imemtia mbaroni na kumfungulia mashtaka kijana huyo aliyejulikana kwa jina la Darwin Martinez Torres mwenye umri wa miaka 22. Katika hali ambayo Waislamu wanaamini kuwa binti huyo aliuawa katika hujuma ya kigaidi ya mtu mwenye chuki dhidi ya Uislamu polisi imepinga mtazamo. Maafisa wa polisi wanasema kifo cha binti huyo aliuawa katika jinai tukio la ‘hasira za barabarani’ au road rage.

Baba wa Nabras, Mohmoud Hassanen, amekanusha vikali madai hayo ya polisi ya Marekani na kusisitiza kuwa, aliuawa kwa kuwa ni Mwislamu.

Hassanen mwenye umri wa miaka sitini alihamia Marekani mwaka 1987 kutoka Misri na marehemu binti yake, Nabra, alizaliwa Marekani na alikuwa binti yake mkubwa miongoni mwa mabanati wannne.

Mauaji ya Nabras yamewashtua Waislamu wa Virginia ambao hukusanyika katika Msikiti wa Adams kwa ajili ya ibada za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Waislamu Marekani wamelalamikia vikali mauaji ya binti huyo Mwislamu na kusema ni kati ya ishara za ongezeko la chuki dhidi ya Waislamu nchini humo.

Tokea Donald Trump aanze kampeani zake za kuwania urais mwaka 2016 na hatimaye kuchukua hatamu za uongozi nchini humo Januari mwaka huu, kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la mashambulio ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Markeani.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani, CARI, mashambulizi yanayowalenga Waislamu nchini humo yaliongezeka kwa karibu asilimia 57 mwaka jana 2016 kutoka kesi 1409 mwaka 2015 na kufikia 2213.

CAIR imetoa wito kwa Waislamu, hasa wanawake wanaovaa Hijabu, kuchukua tahadahri zaidi kutokana na ongezeko la hujuma dhidi yao kote Marekani.

3611460

captcha