IQNA

Mashindano makubwa zaidi ya Qur'ani duniani ya televisheni yafanyika Iran

18:09 - June 25, 2017
Habari ID: 3471035
TEHRAN (IQNA)-Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imerusha hewani mashindano makubwa zaidi duniani ya Qur'ani ya moja kwa moja (live).

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, mashindano hayo ya Qur'ani yamerushwa moja kwa moja na Televisheni ya al-Kawthar, ambayo hurusha matangazo kwa lugha ya Kiarabu.

Televisheni ya Al Kawthar inasimamiwa na Kitengo cha Kimataifa cha Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB. Mshiriki kutoka Iraq ametangazwa mshindi katika mashindano hayo yanajulikana kama,  إِنَّ لِلْمُتَّقِينَ مَفَازًا , "Hakika wachamngu wanastahiki kufuzu". Mshindi huyo Muiraqi amepata zawadi ya dola 5000.

Mshiriki kutoka Iran amepata nafasi ya pili akifuatiwa na Mmisri, Muafghanistani na Mlebanoni ambao wamepata zawadi za dola 4000, 3000, 2000, na 1000 kwa taratibu.

Mashindano hayo yamefanyika katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani na kila kipindi kilikuwa kikichukua lisaa limoja na nusu.

Kwa mujibu wa taratibu za mashindano hayo, washiriki wanaweza kufika katika studio za televisheni ya Al Kawthar na wasioweza wanashiriki kwa njia ya simu. Majaji katika mashindano hayo walikuwa ni kutoka Misri, Syria, Iraq na Iran. Washiriki 24 walifika nusu fainali ambapo watano walishiriki katika fainali ambayo ilifanyika Jumamosi usiku ambayo ilikuwa siku ya Mwisho ya Mwezi wa Ramadhani katika baadhi ya nchi za Kiislamu. Mashindano hayo pia yalirushwa hewani moja kwa moja na Kanali ya Televisheni ya Qur'ani ya Shirika la Utangazaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Mashindano makubwa zaidi ya Qur'ani duiani ya televisheni yafanyika Iran


Mashindano makubwa zaidi ya Qur'ani duiani ya televisheni yafanyika Iran

/3613040

captcha