IQNA

Sala Kubwa Zaidi ya Idul Fitr Barani Ulaya yasaliwa Birmingham, UK+ PICHA

11:34 - June 27, 2017
1
Habari ID: 3471038
TEHRAN (IQNA)-Zaidi ya Waislamu zaidi ya 100,000 wameshiriki katika Sala ya Idul Fitr Jumapili katika bustani moja Uingereza na kuufanya mjumuiko huwa kuwa mkubwa zaidi wa sala ya Idi barani Ulaya.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Waislamu wa kutoka mataifa mbali mbali duniani walishiriki katika Sala ya Idul Fitr iliyosaliwa katika Bustani ya Small Heath mjini Birmingham Uingereza.

Maafisa wa usalama walionekana wakilinda doria kuzuia hujuma dhidi ya Waislamu kama  iliyoshuhudiwa hivi karibuni katika Msikiti wa Finsbury mjini London ambapo Mwislamu aliuawa kwa kukakanyagwa na gari baada ya sala ya Tarawih.

Walioandaa sala hiyo ya Idul Fitr wamekadiria kuwa zaidi ya waumini 106,000 walishiriki katika sala ibada hiyo ya kuashiria kumalizika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Huu ni mwaka wa saba tokea Sala ya Idul Fitr ianze kusaliwa katika Bustani ya Small Heath ambapo mwaka 2012, Waislamu 12,000 walishiriki . Msikiti wa Green Lane huandaa sala hiyo ambayo inashuhudia ongezeko la wanaoswali kila mwaka.

Msikiti wa Green Lane umetoa taarifa na kusema: "Sherehe ya Idul Fitr ni moja ya sherehe muhimu zaidi katika Uislamu na ni fursa ya sote kukutana kwa amani na umoja."

Mkurugenzi wa Msikiti wa Green Lane Amer Ijaz amesema sala hiyo imeandaliwa kwa ushirikiano wa misikiti mingine mitano na shirika la Kiislamu la kutoa misaada la Human Appeal. Baada ya sala kulikuwa na michezo na tafrisha mbali mbali hasa kwa ajili ya watoto.

Indakadiriwa kuwa kuna Waislamu milioni tatu kati ya watu wote milioni 65 nchini Uingereza.


Sala Kubwa Zaidi ya Idul Fitr Barani Ulaya yasaliwa Birmingham, UK+ PICHA


Sala Kubwa Zaidi ya Idul Fitr Barani Ulaya yasaliwa Birmingham, UK+ PICHA


Sala Kubwa Zaidi ya Idul Fitr Barani Ulaya yasaliwa Birmingham, UK+ PICHA


Sala Kubwa Zaidi ya Idul Fitr Barani Ulaya yasaliwa Birmingham, UK+ PICHA


Sala Kubwa Zaidi ya Idul Fitr Barani Ulaya yasaliwa Birmingham, UK+ PICHASala Kubwa Zaidi ya Idul Fitr Barani Ulaya yasaliwa Birmingham, UK+ PICHA



3613563

Imechapishwa: 1
Inatathminiwa: 0
Haiwezi kuchapishwa: 0
Yasin Said
0
0
Mashaallah!
captcha