IQNA

Algeria yasambaza Nakala za Qur'ani nchini Russia

11:30 - June 28, 2017
Habari ID: 3471039
TEHRAN (IQNA)-Algeria imetoa msaada wa mamia ya nakala za Qur'an Tukufu kwa ajili ya Waislamu nchini Russia.

Kwa mujibu wa Shirika Rasmi la Habari la Algeria, nakala hizo za Qur'ani zimezawadiwa misikiti na vituo vya kidini mjini Moscow na pia eneo la Siberia na maeneo ya Mashariki mwa Mbali nchini Russia.

Sherehe za kukabidhi nakala hizo za Qur'ani zilizochapishwa Algeria zimefanyika katika sherehe iliyohudhuriwa na wanazuoni wa Kiislamu Russia na maimamu wa Sala ya Ijumaa.

Ubalozi wa Algeria mjini Moscow umesema Wizara ya Waqfu na Masuala ya Kidini Algeria imetoa mchango huo kama sehemu ya uhusiano wa kistratijia na Russia.

Katika miaka ya hivi karibuni Algeria imeimarisha uhusiano wake na vituo vya Kiislmau nchini Russia.

Idadi ya Waislamu nchini Russia inakadiriwa kuwa ni milioni 20 kati ya watu milioi 144 nchini humo.

3613208

captcha