IQNA

Maombolezo baada Saudia kumuua mwalimu wa Qur'ani huko Qatif

18:56 - July 01, 2017
Habari ID: 3471044
TEHRAN (IQNA)-Waislamu wa eneo la Qatif nchini Saudi Arabia wanaombolezo mauji ya kidhalimu mwalimu wa Qur'ani Tukufu, Amin al Hani, aliyepigwa risasi na kuuwa shahidi na wanajeshi wa utawala wa kiimla wa Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, katika hali ambayo Jumamosi 24 Juni wiki iliyopita Waislamu kote duniani waikuwa wakikaribia kumaliza Saumu ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhani huku wakijitayarishwa kwa ajili ya Siku Kuu ya Idul Fitr, Waislamu wa Saudia hasa Waislamu wa madhehebu ya Shia eneo la Qatif walishuhudia jinai ya wanajeshi wa utawala wa Saudi Arabia ambao walimuua shahidi kidhalimu mwalimu na mwanaharakati wa Qur'ani Tukufu Amin al Hani.

Tukio hilo lilijiri Jumamosi usiku wakati wanajeshi walipofyatulia risasi gari la Amin al Hani akiwa analiendesha katika mji wa Awamiyah ulio eneo la Qatif lenye wakaazi wengi Waislamu wa madhehebu ya Shia. Baada ya gari hilo kufyatuliwa risasi liliteketea moto na baadaye mwili wa marehemu al Hani ulipatikana ndani ya gari hilo. Ilibidi wataalamu watumie mbinu ya kupima vinasaba (DNA) ili kuutambua mwili wa Shahidi Hani, haukuweza kutambulika kutokana na moto mkali uliomteketeza.

Video ya tukio hilo imeenea katika mitandao ya kijamii na kuibua hasira ya wakaazi wa eneo hilo.

Shahidi Hani alikuwa pia mwenyekiti wa baraza la Qur'ani katika mji Awamiya katika eneo la Qatif na wanajeshi katili wa ufalme wa Saudia walimuua shahidi akiwa anarejea kutoka katika majlisi ya Qur'ani Tukufu.

Maulamaa wa Kishia nchini Saudi Arabia wamebainisha masikitiko yao makubwa kufuatia kuuawa shahidi Ustadh Hani na kusema ameacha pengo kubwa sana katika jamii ya watu wa Qatif na Saudi Arabia kwa ujumla. Kutokana na nafasi yake katika harakati za Qur'ani, Hani ametajwa kuwa Shahidi wa Qur'ani. Mauaji ya msomi huyo wa Qur'ani Tukufu ni sehemu nyingine ya jinai zisizo na kikomo za ukoo wa Aal Saud ambao unakali ardhi ya Hijaz iliyopachikwa jina la Saudi Arabia.

Maombolezo baada Saudia kumuua mwalimu wa Qur'ani huko Qatif

Maombolezo baada Saudia kumuua mwalimu wa Qur'ani huko Qatif


3614009
captcha