Safari ya Modi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavuna Wazayuni imetajwa kwa mtazamo wa duru za habari na kisiasa kuwa ni safari ya kihistoria kwa kuwa huyo ni Waziri Mkuu wa kwanza wa India kufanya ziara kama hiyo.
Imeelezwa kuwa India katika miaka ya hivi karibuni ilisaini pia makubaliano ya kiuslama kati yake na utawala wa Kizayuni.
Safari ya Narendra Modi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu ni jambo lililotabiriwa kwa kuzingatia uhusiano wa karibu sana uliopo kati ya Taasisi yenye Misimamo ya Uchupaji Mipaka ya Kihindu ijulikanayo kwa jina la RSS na utawala wa katili wa Kizayuni wa Israel.
Chama cha kibaniani cha BJP kimeimarisha uhusiano na Israel
Uhusiano kati ya India na utawala haramu wa Kizayuni unaoikalia Quds Tukufu kwa mabavu umekuwa ukistawi katika nyanja zote hususan katika masuala ya usalama na makombora tangu mwaka 2014 kilipoingia madarakani huko India chama cha Kibaniani chenye misimamo mikali ya Kihindu cha Bharatiya Janata (BJP). Hadi kufikia mwaka 1992 pande mbili India na utawala wa Kizayuni zilikuwa na mahusiano ya siri. Kimsingi viongozi wa serikali ya hivi sasa ya India hususan wa chama tawala cha BJP wameamua kuanzisha uhusiano na Wazayuni maghasibu kwa malengo kadhaa. Lengo la kwanza lilikuwa ni kustafidi na uzeofu wa kiukandamizaji unaofanywa na Wazayuni watenda jinai wanaowakandamiza kwa kila namnaWapalestina ili kuwakandamiza na kuzima harakati za ukombozi za raia wa eneo la Kashmir linalodhibitiwa na India. Aidha hatua ya utawala huo ya kutumia zana za kijeshi na kiusalama ikiwemo kutumia silaha za balistiki dhidi ya waandamanaji imezidisha ukandamizaji wa askari eti wa usalama wa India dhidi ya raia wa eneo la Kashmir; hatua ambayo imekabiliwa na malalamiko na upinzani wa hata serikali ya ndani ya eneo hilo.
Suala la silaha za nyuklia
Lengo la pili la New Delhi la kuimarisha uhusiano wake na utawala wa Kizayuni wa Israel ni kwa ajili ya kustafidi na uwezo wa utawala huo wa kuendeleza maghala ya nyuklia na makombora ya India; nchi ambayo inashindana vikali na Pakistan na China katika uwanja huo. Lengo la tatu lililoipelekeaserikali ya India kuimarisha uhusiano na utawala wa Kizayuni ni kutaka kustafidi na lobi ya Wazayuni huko Marekani ili ziisaidie India kukuza uhusiano wake na Marekani. Lengo la nne la New Delhi linatajwa kuwa ni kutaka kuwa na sauti zaidi katika eneo hili kwa kushirikiana na utawala wa Kizayuni sambamba na kuimarisha nafasi yake ya kijeshi na kiusalama mkabala na China na Pakistan. Duru za habari na kisiasa zinaamini kuhusiana na hatua hizo za India kwamba serikali ya nchi hiyo inagharimika pakubwa na vile vile inalisababisha eneo hili hasara na maafa makubwa zaidi katika vitendo vyake vya kujipendekeza kwa viongozi watenda jinai wa utawala wa Kizayuni. Madhara makubwa zaidi ya hatua hizo za India ni kuuweka hataraini usalana na umoja wa kitaifa hususan wa india yenyewe.
Ephraim Enbara, Mkuu wa zamani wa Kituo cha utafiti wa Kiistratejia cha Utawala wa Kizayuni amesema kuhusiana na suala hilo kwamba: Uhusiano kati ya India na Israel ni zaidi ya kufikiwa makubaliano ya kiulinzi na kijeshi. Amesema, pande mbili hizo zina malengo ya pamoja ya kiistratejia kama eti ya kuendesha mapambano dhidi ya makundi yenye misimamo ya kufurutu ada, na kwamba pande hizo eti zinahofia nafasi iliyo nayo China na hatari ya nchi hiyo kuwa taifa kuu lililonawiri kiuchumi. Ephraim ameongeza kuwa, India ni soko muhimu la bidhaa za utawala wa Kizayuni wa Israel.
Waislamu India
Wakati huo huo Maulana Tariq Bekhari ambaye ni mmoja wa wajumbewa Jumuiya ya Maulamaa ya India anaamini kwamba: Kuwa na uhusiano wa kiuchumi na utawala wa Kizayuni ni sawa na kushiriki katika mauaji ya watoto, wanawake na raia wasio na hatia wa Palestina. Utawala wa Kizayuni hadi sasa umeshauwa kwa umati maelfu ya raia wa Palestina na haifai kuona nchi yenye viongozi wakubwa kama Mahatma Gandhi na Jawaharlal-Nehru inakuwa na mahusiano na utawala ghasibu wa Kizayuni. Naye Dakta Dhafar Islam mjumbe wa Jumuiya ya Maulamaa wa India ameitaka serikali ya India iheshimu matakwa ya wananchi wake wanaochukizwa na uhusiano wa nchi hiyo na utawala wa Kizayuni. Kivyovyote vile ni wazi kuwa safari ya Narendra Modi, Waziri Mkuu wa India katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu itaanzisha duru mpya ya mashindamo ya silaha katika eneo hili. Utawala wa Kizayuni pia unaamini kuwa kuimarisha uhusiano wake na India ni hatua muhimu ya kustawisha satwa yake katika eneo la Bara Hindi.Ni kwa sababu hiyo ndio maana duru za kisiasa nchini India na katika eneo hili zimekuwa zikiwatahadharisha viongozi wa New Delhi kuhusu taathira mbaya za kuwepo mahusiano ya pande mbili hizo.