IQNA

Maimamu Ulaya waanzisha kampeni ya amani, watembelea miji iliyoathiriwa na ugaidi

21:05 - July 09, 2017
Habari ID: 3471057
TEHRAN (IQNA)-Maimamu wa misikiti barani Ulaya wameanzisha kampeni amani kwa kutemeblea miji iliyoshambulia na magaidi kwa jina la dini huku wakilaani ugaidi na misimamo mikali.

Kwa mujibu wa mwandishi wa IQNA, Maimamu hao kutoka miji kadhaa ya Ulaya walianzia safari yao ya basi Jumamosi mjini Paris wakieneza ujumbe kuwa Uislamu ni dini ya amani. Safari hiyo ya siku sita imepewa jina la "Matembezi ya Waislamu wanaopinga ugaidi". Msafara huyo umeanza katiak eneo la Champs-Elysees mjini Paris, sehemu ambayo afisa wa polisi aliuawa na magaidi miezi kadhaa iliyopita.

Maimamu hao pia wanalenga kubadilisha nyoyo za vijana Waislamu barani Ulaya ambao wamechukua mkondo potovu wa misimamo mikali na utumiaji mabavu huku wakisisitiza kuwa mafundisho ya Kiislamu hayawezi kutumiwa kutetea ugaidi hata kidogo.

Siku ya Jumapili maimamu hao walifika katika mji wa Berlin ambapo walitembelea Kanisa la Kaiser Wilhelm ambalo Disemba mwaka 2016 lilikabiliwa na hujuma ya kigaidi pale mtu aliyekuwa akiendesha gari alipowkanyaga watu waliokuwa katiak soko la Krismasi na kuua 12 kati yao na kuwajeruhi wengine wengi kujeruhiwa. Maimamu hao pia wanatemebelea maeneo yaliyohujumiwa na magaidi huko Brussels Ubelgiji, Tolouse na Nice Ufaransa kabla ya kurejea tena Paris Ijumaa 14 Julai kwa munasaba wa Siku ya Bastille ambayo ni siku ya kitaifa ya Ufaransa.

Viongozi wa Kiislamu walio katika msafara huo wanawaombea pia waathirika wa ugaidi kama njia ya kuonyesha kuwa Waislamu na wafuasi wa dini zingine wanaweza kuishi kwa maelewano na amani. Katika safari yao hiyo, viongozi hao wa Kiislamu pia wanakutana na viongozi wa dini zinginezo, wanasiasa na wanaharakati wa haki za binadmau katika jamii zote zilizoathariwa kwa ugaidi.

Viongozi wa Kiislamu barani Ulaya wanajitahidi kusafisha taswira ya Uislamu iliyoharibiwa na makundi kama vile ISIS ambayo yameuteka na kuudhulumu Uislamu na kutekeleza jinai kwa jina la dini hii tukufu.

"Tunalaani ugaidi kikamilifu ugaidi na tumeimarisha jitihada za mazungumzo na maelewano baina ya wafuasi wa dini mbali mbali." Alisema Abdallah Zekri mmoja wa washiriki katika msafara huo.

Maimamu Ulaya waanzisha kampeni ya amani, watembelea miji iliyoathiriwa na ugaidi


Maimamu Ulaya waanzisha kampeni ya amani, watembelea miji iliyoathiriwa na ugaidi

3463305

captcha