IQNA

Msikiti wahujumiwa tena huko Tennnesse Marekani

10:39 - July 11, 2017
Habari ID: 3471061
TEHRAN (IQNA)-Watu wenye chuki dhidi ya Uislamu wameuhujumu kwa mara nyingine msikiti katika jimbo la Tennessee nchini Marekani.

Taarifa zinasema usiku wa kuamkia Jumatatu watu wenye chuki dhidi ya Uislamu walishambulia Kituo cha Kiislamu cha Murfreesboro na kubandika nyama za nguruwe mlangoni huku wakiandika maandeshi machafafu na yenye matusi katika ukuta wa msikiti na uwanja wa basketboli msikitini hapo.

Msikiti huo ulifunguliwa mwaka 2012 ambapo wakati wa ujenzi wake ulihujumiwa pia mara kadhaa.

Katika taarifa msemaji wa Kituo cha Kiislamu cha Murfressboro amesema Saleh Sbenaty : "Tumeshtuliwa na kusikitishwa na kitendo hiki cha chuki dhidi ya Waislamu na hujuma dhidi ya jengo letu la ibada na kituo cha kijamii.” Aidha amewashukuru majirani kwa kuonyesha mshikamano baada ya tukio hilo.

Kamanda wa polisi katika eneo hilo Dan Goodwin amesema uchunguzi unafanyika kuhusu kitendo hicho cha jinai huku akisema wanatafuta taarifa kuhusu watu ambao wanaweza kuwa wamezungumza kuhusu kuuvunjia heshima msikiti huo.

Kituo cha Kiislamu cha Murfreesboro kimekuwa na historia ndefu ya kuhujumiwa kwa zaidi ya muongo moja. Awali kituo hicho kilikuwa katika jengo moja ndogo katika eneo la Tennessee Boulevard. Mwaka 2010 jaji katika Kaunti ya Rutherford aliafiki ujenzi wa msikiti na kituo kipya cha Kiislamu katika eneo la sasa la Barabara ya Veals. Baada ya uamuzi huo baadhi ya watu wenye chuki dhidi ya Waislamu walipelekea kesi kortini wakitaka ujenzi usitishwe lakini wakasindwa. Kituo cha sasa kilifunguliwa Agosti 2012 na bado ujenzi wake unaendelea ili kujumuisha viwanja vya michezo. Mwaka 2011 msikiti huo ulipokea tishio la bomu na pia baada ya kufunguliwa ulihujumiwa.

Tokea Donald Trump aanze kampeani zake za kuwania urais mwaka 2016 na hatimaye kuchukua hatamu za uongozi nchini humo Januari mwaka huu, kumeshuhudiwa ongezeko kubwa la mashambulio ya chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu Markeani.

Baraza la Mahusiano ya Kiislamu nchini Marekani, CARI, mashambulizi yanayowalenga Waislamu nchini humo yaliongezeka kwa karibu asilimia 57 mwaka jana 2016 kutoka kesi 1409 mwaka 2015 na kufikia 2213.

CAIR imetoa wito kwa Waislamu, hasa wanawake wanaovaa Hijabu, kuchukua tahadahri zaidi kutokana na ongezeko la hujuma dhidi yao kote Marekani.

3463323

captcha