IQNA

Mmalaysia aandaa ‘Saa ya Qu’rani Duniani’ Agosti 31

0:01 - August 07, 2017
Habari ID: 3471109
TEHRAN (IQNA)-Mkurungenzi mmoja wa sanaa nchini Malaysia ameandaa Saa ya Qur’ani (#QuranHour) kwa lengo la kuwakumbusha walimwengu wote kuhusu mvuto wa mafundisho ya Qur’ani Tukufu.

Datuk Rosyam Noor amesema atatumia harakati hiyo, ambayo katika mitandao ya kijamii inajulikana kama World #QuranHour, kwa lengo la kuleta umoja katika jamii zote nchini humo.

Amesema kuna fikra potovu kuhusu Uislamu ambapo baadhi wanadhani kuwa Waislamu ni watu wapendao vita na ghasia. ‘Harakati hii inalenga kuondoa fikra mbaya kuhusu Uislamu. Tunataka watu wafahamu kuwa dini haiwezi kunasibishwa na tabia za watu wachache.”

Amesema wasiokuwa Waislamu wanakaribishwa katika harakati hiyo ya ili washuhudie mvuto uliopo katika mafundishi ya Qur’ani Tukufu.

Aidha amesema harakati haiyo ya World #QuranHour itafanyika Agosti 31, kwa minasaba miwili. Awali siku hiyo inatazamiwa kuwa Mahujaji katika Ibada ya Hija watakuwa wakitekeleza amani ya Wukufu huko Arafah na pili Agosti 31 pia ni Siku ya Kitaifa ya Malaysia.Mmalaysia aandaa ‘Saa ya Qu’rani Duniani’ Agosti 31

Shughuli hiyo ya World #QuranHour itafanyika katika Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kiislamu Malaysia katika Msikiti wa Sultan Haji Ahmad Shah kuanzia saa tano asubuhi hadi saa saba mchana kwa wakati wa nchi hiyo ya Kusini Mashariki mwa Asia.

3463563

captcha